Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Kwa wenzetu,muundo wa gari lilotumika,rangi yake ni lead tosha kabisa,undefinedmaana gari zote za muundo huo zitaorodheshwa na wataanza kunarrowdown hadi wanapata connection
 
Hili suala la mo limeivua serikali na polisi nguo kabisa.Probably hata uwezo wa kutafuta watu hawana so huko nyuma walikuwa wanaongea porojo ila ukweli umedhihirika kwa hili la mo usalama wa wananchi uko mikononi mwetu tusitegemee polisi wala serikali kufanya lolote.
Inakuwaje bilionea anapotea kirahisi hivi kwenye mazingira yale hatua chache wako 'suti',majumba ya viongozi wakubwa wakubwa hivi mwananchi alieko nyambureti atasemaje yuko salama????????????
 
Na hii mizaha hawataacha hadi pale kiongozi mmoja mkubwa sana atakapohifadhiwa kwa muda sehemu isiyojulikana.

Dreka,
They 've got it coming!
Walianza mizaha na kupuuza kila utekaji unapotokea kuwa unawahusu WAPINZANI!!Hakika mficha maradhi msiba utamwumbua!Yalikuwa yana kina Lissu,Ben,Azory,Wangwe,etc!Leo liko kwa Mo Dewji...who will be next?
 
Hatujamsahau yaani mi nalogin mitandao kuliko muda wowote japo nione habari njema ila hola binafsi sijawahi muona physically ila kaniumiza sana sana utadhani ndugu wa karibu .kweli dunia ni katiri sometimes
 
Wakianzia na konda inaweza kuwa vzr zaidi

I don trust this kondakta!
Angalia anavojichanganya kuhusu Mo issue!Mara aseme Mo keshapatikana yuko salama mara hajapatikana mara tutampata Mo akiwa salama kana kwamba anajua yuko mahali fulani....!!l wish I could be IGP!Konda angelikuwa suspect No.1!!!!

Ukiunganisha na matukio ya wale wanamuziki waliotekwa na konda akasema watapatikana ndani ya 2 days wakiwa salama salmin na ndivo ilivotokea!
Kuna watawala wako tayari kuumiza jamii ili kujikweza kisiasa.......nonsense!!
 
Dreka,
They 've got it coming!
Walianza mizaha na kupuuza kila utekaji unapotokea kwa unawahusu WAPINZANI!
Hakika mficha maradhi msiba utamwumbua!Yalikuwa yana kina Lissu,Ben,Azory,Wangwe,etc!Leo liko kwa Mo Dewji...who will be next?


Nchi yetu Tanzania is now no longer a heaven of peace! Wanasiasa na Watawala wetu ndio Chablis na sababu ya kuanza kutoweka kwa Amani ya nji hii tuliyoachiwa na Mwasisi na Baba wa Taifa letu hayati Nyerere!
Kila kunapotokea tukio baya kama hili la kutekwa na kupotea kwa Mo Dewji ni kawaida kuona Watawala wakitoa matamko ambaye mara nyingi hayana tija na mara mara nyingi ni ya kisiasa zaidi kuliko weledi na uhalisia wa tukio lenyewe!

Mfano: Ben Saanane alipotekwa na kupotea katika mazingira ya kutatanisha,mwajiri wake CHADEMA alipoanza kuhoji kupotea kwa Ben zikaingizwa siasa ya kwamba CHADEMA wenyewe ndio wanajua alipo!
Kuna watawala walidiriki kusema BEN SAANANE AMEJITEKA mwenyewe!
Lugha na matamko kama haya ni hatari sana kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu!

Azory Gwanda alitekwa na watu wasiojulikana yamesemwa mengi na Wanasiasa na Watawala!Kwamba anajua alipokwenda kwa vile alimwaga mkewe!Lakini mpaka leo hajapatikana! Tundu Lissu kapigwa risasi 38 mchana kweupe na watu wasiojulikana mpaka hawajajulikana wala hakuna mtuhumiwa hata mmoja!CHADEMA na Watanzania wakihoji kwa Polisi na Watawala lawama zinatupwa kwa waathirika CHADEMA kwamba wao ndo wanahusika kwasababu ya ugomvi wa kisiasa ndani ya chama au ni visasi vya kibiashara!!!Swali linakuja kama ni CHADEMA wanahusika kwanini hawakamatwi na kushtakiwa?

Wakti Chacha Wangwe alipokufa kwa ajali ya gari,habari zikaenezwa na Wanasiasa na Watawala kwamba CHADEMA ndo wanahusika na ajali maana Wangwe alikuwa akitaka kugombea Umwenyekiti wa CHADEMA..!!Kila tukio la kufa au kupotea kwa Mtz na hasa kama ni kutoka Upinzani itatengenezwa picha au maigizo ya kuchanganya raia!

Vyombo vya ulinzi na Usalama vimegeuzwa kuwa ni vyombo vya kulinda na kutetea uongo wa Wanasiasa na hivo kupoteza weledi wao wa kuhakikisha Usalama wa kila Mtz!Kwa adui yeyote mwenye nia mbaya anaweza kutumia udhaifu huu kufanya anavotaka!Kwamba sasa imefikia RAIA WA KIGENI TENA WAZUNGU AU SIJUI NI WAHINDI,WACHINA au nchi gani wamediriki kuvuka mipaka na kuingia chumbani na kufanya uhalisi na kutoka salama salmin kana kwamba nchi imelala usingizi!
Lazima tubadilike otherwise nchi iko katika hatari ya kuvamiwa na adui toka nje na ndani wakti wowote!!!


Ndugu yako huyu huku anapewa kibano na Wahindi wewe unampigania Muhindi? Ni lazima utakuwa mgonjwa wa akili au labda umekulia uhindini umelelewa huko?

 
Tutaendelea kumtafuta MO na kuhakikisha watanzania wanapata majibu sahihi na majibu sahihi ni kwamba MO AMEPATIKANA NA WATEKAJI WAKE WAMEKAMATWA.

Tusipende ku twist maneno ili kufurahisha watu.
 
Kwa wenzetu,muundo wa gari lilotumika,rangi yake ni lead tosha kabisa,undefinedmaana gari zote za muundo huo zitaorodheshwa na wataanza kunarrowdown hadi wanapata connection
We nchi zetu bado tech ya wenzetu balaa niona juzi wanavyotumia image ku link hadi kupata passport photo ya mharifu sina uhakika kama tumefika hata robo. Kwetu nahsi wakichoka wanafunga file wenzetu hata second generation wanatoa data kama issue ni.mpya ili haki itemdeke
 
Tujiulize kama waliweza kuwapata au kutowapata waliomshambulia Lissu, waliomteka Roma, waliomteka Azory, waliompoteza Benny, waliomuua Akwilina, waliomteka na kumtesa Dr Ulimboka, walio muua Mawazo, waliomdhuru Kibanda, watu wanakutwa wamefungwa kwenye viroba nk Tukipata jibu ndio jibu la kutekwa kwa Mo
 
Hebu Ngoja nikae kimya nisije nikakufuru
Mtu akipotea mitaani pamoja na kuripoti polisi spika misikitini hutangaza kuwa yeyote atakayemwona apeleke taarifa kituo cha polisi au msikitini nk Kupotea mtu si kitu cha kuachia polisi tu
 
Tutaendelea kumtafuta MO na kuhakikisha watanzania wanapata majibu sahihi na majibu sahihi ni kwamba MO AMEPATIKANA NA WATEKAJI WAKE WAMEKAMATWA.

Tusipende ku twist maneno ili kufurahisha watu.
Hii kauli ni tata sana maana aliitoa lakini nafikiri ilikuwa ni kutuliza, japo kwa muda mfupi, mzuka wa wananchi.

Ila DAB aliwahi kusema Roma mkatoliki atapatika, na akapatikana. Mo pia atapatikana kwa neno la kiunabii la DAB!
 
Tutaendelea kumtafuta MO na kuhakikisha watanzania wanapata majibu sahihi na majibu sahihi ni kwamba MO AMEPATIKANA NA WATEKAJI WAKE WAMEKAMATWA.

Tusipende ku twist maneno ili kufurahisha watu.
True ndo alichomaanisha kuwa majibu sahihi yawe ni...amepatikana....Sio kuwa amepatakina
 
Back
Top Bottom