Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Mbona wasiojulikana waliomshambulia Lissu hawakuwa wamevaa mask na CCTV ziling'olewa muda mfupi baada ya Lissu kushambuliwa lakini hadi leo upelelezi haujaanza? Mkuu usitetee wauaji pasipo kutumia akili.
Sasa unaniuliza mimi kuhusu wahuaji wa Lissu kwani mimi niliwaona?

Halafu mimi napojibu hoja situmii maneno ya watu mtaani....mimi nasema kulingana na ripoti ya polisi.

Wewe ulijuaje kwamba hawakuvaa mask?Ulikuwepo kipindi cctv zinachukuliwa?
Ni lini ambapo shuhuda wa tukio au mhusika alihojiwa kwa ajili ya upelelezi?

Halafu maelezo yangu ya hapo juu ni wapi nimetetea wahalifu. Au unaandika tu kwa sababu unajua kuandika?

Mimi sio CHADEMA wala CCM siendeshwi na ulevi wa vyama vyenu hivyo...mimi najitegemea katika kuchambua mambo

Siendeshwi na hisia za wengi naendeshwa na akili yangu niliyopewa ya kupambanua mambo. Nadhani umenisoma.

ASANTE
 
Sasa unaniuliza mimi kuhusu wahuaji wa Lissu kwani mimi niliwaona?

Halafu mimi napojibu hoja situmii maneno ya watu mtaani....mimi nasema kulingana na ripoti ya polisi.

Wewe ulijuaje kwamba hawakuvaa mask?Ulikuwepo kipindi cctv zinachukuliwa?
Ni lini ambapo shuhuda wa tukio au mhusika alihojiwa kwa ajili ya upelelezi?

Halafu maelezo yangu ya hapo juu ni wapi nimetetea wahalifu. Au unaandika tu kwa sababu unajua kuandika?

Mimi sio CHADEMA wala CCM siendeshwi na ulevi wa vyama vyenu hivyo...mimi najitegemea katika kuchambua mambo

Siendeshwi na hisia za wengi naendeshwa na akili yangu niliyopewa ya kupambanua mambo. Nadhani umenisoma.

ASANTE
Kajamaa kanaboa haka. 'Namaanisha wewe' halafu utakuta kamesoma, tena labda kapo kitengo. But ni keupe kichwani kama rangi ya magogoni.
 
Mipango dhalimu ya wasioitakia mema Tanzania... Tuendelee kuomba atapatikana yuhai
 
Rais mnamlahumu nini? Masaa yote mnaleta mambo ya siasa. Rais atajiingizaje kwenye mambo ambayo yamekaa ndio sivyo, haijulikani kama mambo yenyewe ni maiigizo for some reason au yana ukweli.

Nimejaribu kutafakali tukio zima nikaona mambo mengi don't seems to add up at all, hivi inaingia akilini kwamba watu ambao wako determined kuteka MTU watamsubilia aingie kwenye eneo ambalo kuna watu wengi,CCTV cameras na smartphones za ku-record matukio, in other words atekwe sehemu ambayo publicity ya tukio zima itakuwa na impact kubwa, kwa nini hakutekwa akitoka geitini kwake au akiwa njiani kuelekea kwenye gym, si wanasema ana kawaida ya kujiendesha mwenyewe - watekaji gani wanaweza kujitumbukiza sehemu ambayo wangeweza kuwa cornered kirahisi au kukamatwa na askali wa Doria??

Sina nia mbaya ya kuwasema vibaya wafanya biashara, lakini kumbuka kuna wengine ambao unaweza kukuta wanajingiza kwenye mambo ambayo kwa akili za kawaida si rahisi kuamini - niliwahi kushuhudia mifano kadhaa huko Ulaya na US - Siku mmoja kulitolewa habari kwamba mfanya biashara mkubwa aliye kuwa anamiliki magazeti ya the Mirror, Club ya mpira ya Chelsea,Kampuni kubwa ya bima kwa wastaafu nk eti alipotea baada ya kuteleza na kutumbukia baharini wakati akivinjari baharini na Yatch yake!! Polisi wali angahika sana kutafuta mwili wake bila mafanikio,baadae wapelelezi wakatilia shaka upotevu wake wakalazimika kufatilia nyenendo za makampuni yake, mambo waliyo gundua huko siwezi kuyarudia hapa, MTU mwenyewe alikuwa mwenye asili ya kiyahudi baadae ikaja gundulika kumbe alikimbilia huko na kubadiri sura!

Nisije kueleweka vibaya kwamba labda sikusikitishwa na utekwaji nyara wa mzalendo mwenzetu Mr.Mo, far from it - ninacho shauri vyombo vya Dola zichunguze kwa kina kwa uzito ule ule pande zote mbili i.e personal na washindani wake.
Kama ni drama, kwanini basi drama hiyo isifanyike huko unakodhani kama ni utekaji wa kweli ndo ungeweza kufanyika pasipo na risk?! Kwa sababu, drama ya kutekwa ingefanyika succesfully bila ya kuwa na hofu ya conuterattack na badala yake drama hiyo wanaenda kuifanya eneo ambalo kuna risk ya kuhatarisha filamu mzima!!!

Kuweka kumbukumbu sawa, hata Ben Saanane wapo waliosema amejiteka (drama)! Wkati taarifa za awali kuhusu Lissu kupigwa risasi, wapo pia waliosema ni kiki! ROMA nae watu walisema ni kiki! Naona nawe unajaribu kupita mle mle!
 
HUU MCHEZO MBAYA SANA, STOP 🛑 IT PLEASE.
WE ARE HERE ON EARTH [emoji288] FOR A SEASON.
BRING BACK OUR MO
 
Nasikitika kusema poliCCM ni majitu ya ajabu sana ktk nchi hii.Iweje mtu atekwe sasa ni siku ya 3 lakini hakuna fununu yoyote juu ya mahali aliko Mo Dewji Hivi nchi hii kweli tunao wapelelezi wanaojitambua au tuna matutusa tu
Tatizo la polisi wa nchi hii ni kukimbilia kutoa taarifa tata mbele ya vyombo vya habari pasipo kutumia akili.Upolisi Paipo Elimu (UPE)ndicho chanzo kikuu cha ukosefu wa weledi miongoni mwa poliCCM.Tazama jinsi ambavyo Mambokale alijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kadi yake ya CCM kuupotosha umma wa watanzania kuhusu watekaji:
  • Watekaji ni wazungu sio raia wan chi hii).Je,ulikagua vitambulisho vyao vya uraia?Je,mtu yeyote mwenye rangi nyeupe ni MZUNGU?
Haikubaliki hata kidogo kutolewa taarifa ya ovyo na potoshi kama hii halafu wananchi tukae kimya ilhali Mo bado hajapatikana. Unless poliCCM mtuambie kwamba mna ajenda ya siri juu ya utekajihuu.
Huu upuuzi wote wanini? Polc wanafanya kila wawezalo kumtafutaMo.
 
Kumbuka kulingana na ripoti ya jeshi la polisi wale watekaji walikuwa wamevaa mask.

Ki kawaida mtu akivaa masiki uwezi ukafahamu sura yake kwa macho ya kawaida ya kamera za cctv.

Kama utakumbuka shambulio la Westgate lilivyokuwa bila shaka utapata picha.

ASANTENI
Mkuu kamera za cctv sio kutambua sura ya mtu peke yake, hata hio gari raia wakionenshwa kupitia hio cctv wataweza kuitambua na kusema labda waliwahi kuiona wapi mara mwisho au kuingia nyumba hipi mara kwa mara.

Haya mambo ni muhimu kuwekwa wazi kama polisi wanataka msaada wa wananchi.
 
Ndugu watanzania kama kawaida yetu wazee Wa matukio

Alianza Ben siku ya kwanza ya pili yavtatu ya nne tukamsahau mpaka Leo mwaka Wa pili unaelekea kuisha Ben hajulikani halipo na tumesahau kabisa

Akafuata Azory siku ya kwanza ya pili ya tatu ya NNE ya tano mpaka Leo azory tumemsahau na maisha yanaendelea

Sasa amefuata bilionea MO siku ya kwanza tukaongea siku ya pili tukaongea siku ya tatu tukaanza kusahau
Siku ya NNE nayo imepita

Kimasihara masihara hivihivi tumeanza kusahau na maisha yameanza kusonga kama kawa

Bado najiuliza Leo siku ya NNE hajapatikana na watanzania wameshaanza kusahau sasa hivi huyu atapatikana kweli au ndio Yale Yale ya akina Ben? Ngoja niishie hapa

TIME WILL TELL
 
Back
Top Bottom