Magufuli ana matendo gani mema? Kuuwa na kutukana watu?. Kujenga madaraka na reli ilikiwa kwenye mpango wa miaka mitano wa serikali sio maono yake.
Magufuli aliamini na alisimamia kwa vitendo mambo yafuatayo:
Kupinga rushwa ili kuboresha huduma za kijamii. Alisimamia na kuweka nidhamu kwa watumishi wa umma hali iliyopelekea wananchi kupata huduma bila usumbufu wa kuashiria rushwa. Katika kupambana na rushwa, Magufuli alikamata wahujimu uchumi, alirudisha ardhi zilizokuwa zimeporwa na mafisadi kutoka kwa wananchi n.k (yako mengi sana)
Kuboresha huduma za kijamii ili watanzania wote wanufaike. Alianzisha sera ya elimumsingi bila malipo hali iliyopelekea udahili wa wanafunzi shuleni kiongezeka maradufu 2016 - 2021 kwa ngazi zote.
Aliamini rasilimali za watanzania ni kwa ajili ya watanzania. Masoko ya madini yalijengwa nchini Tanzania, alidhubiti ujangiri wa wanyama pori ili kulinda hifadhi za wanyamapori kwa ajili ya manufaa ya watanzania.
Aliamini katika ustawi wa jamii ya watanzania kwa kudumisha afya (alijenga hospitali, zahanati na vituo vya afya vingi sana nchini), alidhibiti uuzaji na usambazaji wa madawa ya kulevya nchini kwa kuanzisha taasisi maalumu ya jukumu hilo. Aidha, JP Magufuli alilinda utamaduni wa mtanzania kwa kukemea hadharani ushoga na kupiga ban NGOs uchwara zenye ajenda mbaya za kuharibu utamaduni wa mtanzania.
Magufuli alikuwa mwongozaji aliyejiamini sana bila kuyumbishwa na mtu yeyote. Alitoa misimamo na maono yakuaminika na yenye dira. Hadharani alisema hataki lock down kama njia ya kupambana na Covid 18, hadharani alikataa kutoa takwimu zozote juu ya Covid. Hadharani alitamka CORONA imeisha Tanzania, tukaamini hivyo, na dunia ikafuata msimamo huo; maisha yakaendelea.
Alikuwa muwazi juu ya imani na matumaini yake, alisema kabisa kuwa vita aliyokuwa anaipigana kwa ajili ya watanzania ilikuwa ngumu sana. Alitusihii tumwombee maana maadua walikuwa wengi na wengi hakuwajua. Ni kiongozi aliyeamini katika Mungu; Tanzania ni taifa la Mungu.
Aliamini katika utu. Kwamba kila mtanzania ana haki ya kupata huduma nzuri za kijamii; elimu, afya, mawasiliano na uchukizi. Aliruhusu kila mtu afanye shughuli zake za kiuchumi bila kubugudhiwa. Matching Guys "Machinga" walithaminika kama tabaka la chini la wajasiriamali na walikidhi mahitaji yao ya kimaisha.
Alisimamia wajibu wa kila mtanzania wa kulipa kodi. Kodi ililipwa na kila mtu, miundombinu na miradi mingi sana ya kimaendeleo ilianzishwa na kutekelezwa. Uchumi ulipaa na kuwa "Uchumi wa kati"
Watu wanaposema Magufuli alikuwa ni rais, ni kwa sababu ya haya. Ni haya yanayofanya watanzania waseme hadharani kuwa kwa sasa "Magufulism" ni imani; imani iliyokolea. Na hii ndiyo PHILOSOPHY ya Magufuli.