Hivi kina Membe na Nape walipokimbilia kuanzisha ACT walivurugwa na nini CCM?
Hao jamaa naamini kweli wapo, lakini tatizo linaanzia pale ambapo mara nyingi huwa waoga wa kuweka nia zao wazi, hujificha.
Na huku kujificha kwao naona huchangiwa na tamaa tu, wanatega kutafuta vyeo, wakishavipata wanaachana na mipango yao ya kuanzisha hivi vyama niviite vyama "njaa" na "hasira", wala sio phylosophy kama wanavyosema, ndio maana mara nyingi huwa havi exist, hujifia natural death.
ACT chenyewe hakikufa kwasababu yule msaliti wao waliyemtengeneza toka akiwa Chadema, aliendelea mbele baada ya kujifukuzisha Chadema akakitafutia usajili, ndio akajiita "supreme leader" ila kama naye angeupata ule uenyekiti aliokuwa anautaka Chadema, naamini hiyo ACT nayo leo hii isingekuwepo.