Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni

Serikali ya mama imetoa pesa kwa hiyo mradi unafufuliwa..
 
Kuna uhujumu uchumi zaidi ya huu? Waliouanzinsha na kuutelekeza wanatakiwa kujibu. Hauwezi ku abandon mradi mkubwa namna hii ukaachwa itambe uraiani. Aibu hii!
 
Kipindi cha Kikwete na Kipindi cha Nehemiah Mchechu enzi hizo akiwa DG wa NHC kulikuwa na Miradi mingi sana Mikubwa ya Ujenzi hasa kwa shirika la Nyumba la Taifa karibu kila Pembe ya nchi na yote ilikuwa inakwenda fresh. Baada ya kutolewa sasa...ndo hivyo tena ukimnya na mdororo kwenye miradi ukatanda. Labda amerudishwa Mchechu huenda tukaanza kuona uhai tena
 

Ingependeza sana kama ungeeleza ilikuwa ni upigaji vipi. Kuwa fedha za mradi zilikuwa ni za serikali?? Au Ridhwani na JK hawakuwa na haki ya kuwa na miradi kama hii nk??? Kama unasema kuwa ilikuwa ya upigaji na fedha ni za serikali, si ingekuwa vema kuendeleza miradi hii kwa kuhakikisha fedha zinatumika sahihi? Au unasema mradi haukuwa na maana yoyote zaidi ya faida kwa uliowaita wapigaji?

Roho ya masikini huangalia kwa wivu mambo ya tajiri. Tunapenda sana kuona tajiri ni mtu mbaya - ndio maana sisi tunapenda kuwa na viongozi ambao ni wakulima, wafugaji, watoto wa masikini, wanyonge wenzetu!! Hatutakuja kuwa na viongozi matajiri coz tuna hofu wanatuibia!! Viongozi wenye mawazo yanayotoa faraja kwa wanyonge ili kura ziendelee kupatikana!
 
Sasa ukiusimamisha wakati kuna fedha imeshatumika ndiyo unapata nini? Siyo ndiyo hasara mara mbili??
Mradi uliifilisi NSSF na jiwe naye akachota kiasi NSSF ikajikuta haina pesa za kuwalipa wanachama wake.
 
Kama kulikuwa na ufisadi, ulitakiwa kutaifishwa na wahusika kushtakiwa.
 
Ridhiwani wacha ujinga.....huu mradi unakunufaisha wewe na ukoo wako, it has nothing to do na nchi hii wala wananchi wake. Nyinyi mnaifilisi hii nchi kwa wizi wenu hata kama wewe ungekuwa Magufuli ungefanya hivyo hivyo alivyofanya yeye.
 
Mze (JK) alipiga dili na watu wa nje waliokuwa wanajenga ule mradi.....kwa kuwa yeye alikuwa ndiyo rais akamuweka mtoto wake kuwa CEO wa ule mradi. Mkuu ni story ndefu sana lakini kiufupi tu ule mradi ni wa nchi ni wa Kikwete na familia yake. Wewe, mimi na watanzania wengine hatuna faida nao.
 
Kumbe mradi wenyewe ulikuwa umegubikwa na tuhuma za ufisadi wa mabillioni; ngoja ubaki magofu hivyo hivyo ndo Kikwete na ufisadi wake wajulikane wazi.
 
Jiwe lilikuwa na roho ya Kimaskini Sana.
Hivi hujui fedha zilizokuwa zikitumika kujenga hii mitadi ni fedha za mafao ya waajiliwa na hata walipokuwa wakizidai baada ya kustafu hawakupewa kwa wakati?
Kutoshabikia mambo usiyoyajua ni kuficha upumbaf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…