Mgalula MzTz
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 462
- 421
Ni akili za kipumbaf pia kushangilia miradi kama hii inayotumia pesa za wananchi kujenga nyumba ambazo asilimia kubwa ya watanzania hawawezi kuzimudu kuzinunua, kuna wakati Rais wa awamu ya 5 aliwaeleza viongozi wa haya mashirika kuwa, kwanini wasiwekeze pia hata kwenye miradi mingine kama ya viwanda n.k ili kuwasaidia watz wenye hali duni? au kujenga nyumba za gharama nafuu hasa kwa miji mikubwa kama Dar ili kuwarahisishia watanzania maisha?Utawala wa awamu ta tano ulijenga chuki kati ya Matajiri na Masikini. Tajiri mwenye hela zake alikuwa akikomolewa au kuharibiwa Mali, Masikini wa Tanzania anashangilia. Mfano huu mradi Ulivyo simamishwa, Wananchi walifurahi eti acha wakomolewe. Akili za kimasikini. Mbongo hawezi kukupigia makofu ukifanikiwa au kufanya vizuri. Wanaokupigia makofi ni wale walokaa na watu wa mataifa mengine. Hata mabosi ukifanya vizuri hawawezi kukusifia.
Miradi mingi mizuri nchini huwabagua wasiokuwa nacho na ndiomana Jpm alilipambana kuondoa matabaka na wala sio kuwakandamiza matajiri.
Labda uwataje hapa matajiri waliofilisiwa mali zao kwa chuki bila kuhusika kwenye kashfa za wizi na ukwepaji kodi.
Na pesa za hii mifuko ya hifadhi ni pesa za watu( walipa kodi ) walipozidai baada ya kustafu waliambulia usumbufu mkubwa kwakuwa pesa zao zimeelekezwa kwenye miradi kam hii,wewe unaona ni sawa.
Tuache kutetea mambo ya hovyo ili Taifa lisonge mbele.