Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa hiyo gari ameacha kwenye foleni ikiisha itabaki hapo hapo au kamuachia mtu mwingine arudi nayo home tu ?Msanii Nay wa Mitego amepata ajali ya bodaboda wakati anawahi kwenye Interview ya kipindi cha Friday Night Live cha East Africa TV, kwa sasa msanii huyo yupo katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni akipatiwa matibabu na hali yake bado haiko vizuri.
Taarifa iliyotolewa na EAST AFRICA RADIO inaeleza kuwa Nay alipanda bodaboda ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake. Tutaendelea kutoa taarifa zaidi za maendeleo ya afya yake.
.......................................................
Hivi ni kweli hadi sasa Nay anatumia bodaboda tena usiku kma usafiri? si tuliambiwa na alionesha ana magari mengi sasa imekuwaje?
AminaTunamwombea uponyaji wa haraka
Mmmh ney yuko vizuri weweHuenda ni Kiki mana hawa wasanii ni wasanii kweli kweli , alaf Yale magari yake yako wapi? Au tuamini kauli ya shamsha Ford kwamba jamaa hata pa kulala hana
Kwa jinsi wasanii wanavyorogana si ajabu ajali hii ikahusishwa na uchawiMsanii Emmanuel Eribariki Munis (Nay wa Mitego), amepata ajali ya bodaboda wakati anawahi kwenye Interview.
Kwa sasa msanii huyo yupo katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni akipatiwa matibabu na hali yake bado haiko vizuri.
Inaelezwa alipanda bodaboda ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake.
Hali yake haijatengamaa.
View attachment 1800835