Dar: Msanii Nay wa Mitego amepata ajali ya bodaboda

Dar: Msanii Nay wa Mitego amepata ajali ya bodaboda

Wobongo vituko, sasa kuna kosa gani yeye kuamua kupanda Bodaboda?
 
si ana hela yule bodaboda alipandaje? nimegundua kwa nini jeshini hairuhusiwi afisa wake aande na boda boda
Foleni mkuu. Mara nyingi hata mimi nawahi na boda boda chap
 
Hii habari inaupendeleo, Ney alikuwa anaendesha Pikipiki mwenyewe au alibebwa? Mbona dereva hazungumzwi hali yake kama alimbeba Ney? Au ndiyo yaleyale ya walikuwepo watu watatu na Mmasai mmoja
 
Boda boda ni janga la kitaifa....vijana wanatumia vilevi huku wanaendesha na wenye mamlaka baada ya kuwadhibiti wamewafanya kitega uchumi.......ugua pole msanii....
Yani kuna muda nikiwaangalia vijana bodaboda, najiuliza hivi huyu alipewaje leseni ya kuendesha chombo cha moto? Unakuta dogo anaonekana kabisa bangi zimemkolea,muonekano wa kihuni,uchafu,pombe yani ni balaa.

Kwanini wasiwapime kabla ya kuwapa leseni,Ili kubaini watumiaji wa mihadarati? Serikali iangalie upya juu ya swala la mabodaboda,sawa zinatoa ajira kwa vijana,ila vijana wengine ni wapumbavu tu.
 
Msanii Emmanuel Eribariki Munis (Nay wa Mitego), amepata ajali ya bodaboda wakati anawahi kwenye Interview.

Kwa sasa msanii huyo yupo katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni akipatiwa matibabu na hali yake bado haiko vizuri.

Inaelezwa alipanda bodaboda ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake.

Hali yake haijatengamaa.
View attachment 1800835
pole sana kwetu, atatuponya.
 
Back
Top Bottom