Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Kati ya mambo ambayo ninayahofia baada ya kifo Cha JPM Ni hili la wimi la ujambazi.... Tulikuwa peace hatari
Mama Samia yuko Imara wala usiogope wakianza tu basi dawa yao kama Raisi wa Ruwanda alisema leo nakomesha Ujambazi nchi hii pamoja na wizi alileta kikosi cha Jeshi walikuwa majambazi 4 walipigwa marisasi nyama na mifupa yote ilisambarika kwenye uwanja wa mpira na watu wote mashuhuda basi naam Ruwanda toka siku hiyo mpaka sasa hakuna wezi wala majambazi.
 
Lakini usiku huo muda mfupi kabla ya tatizo hilo la kukutwa amefariki alikuwa anakunywa pombe na rafiki yake pale sokoni Makumbusho stendi na alikuwa amelewa sana(kulingana na wenyeji sokoni ambapo Blandina naye ni mwenyeji mno hilo eneo kwani aliwahi kuwa na jiko la chakula na ana rafiki yake mpendwa)...
Duh. Kwa hiyo story ya Noah, pia boda wanalindana?
 
Lawama zote za utekaji na mauaji tulizitupa kw jiwe hezi za utawala wake,kwa Sasa hatuko nae tena sasa mambo yameanza tena hizi lawama tutamtupia nani au tuanze tena kwa huyu mama?
 
Lakini usiku huo muda mfupi kabla ya tatizo hilo la kukutwa amefariki alikuwa anakunywa pombe na rafiki yake pale sokoni Makumbusho stendi na alikuwa amelewa sana(kulingana na wenyeji sokoni ambapo Blandina naye ni mwenyeji mno hilo eneo kwani aliwahi kuwa na jiko la chakula na ana rafiki yake mpendwa)...
Ajali mjona sio kesi kubwa kama kuhisiwa mauaji?...kuna haja gani kukimbia kesi ya ajali na ukumbane na kesi ya mauaji?
 
Katika kazi sizipendi naziogopa zenye hatari ya kupoteza maisha bila Mungu kupenda ni

1.Usalama (polisi na wanajeshi)
2.Uandishi wa Habari
3.Udereva (wa aina yeyote ile iwe ndege/meli/rocket,nk)

Hizi sekta 3 hizi Mungu apende asipende wanadamu wanaweza amua yao wakafanya kweli.
Unaposema Mungu apende asipende kwa vyovyote lazima uuawe. Hapa utakuwa umemkosea sana Mwenyezi Mungu maana umeonyesha kuwa wanaadam wana nguvu wakitaka lao lifanyike kuliko anavyotaka Mwenyezi Mungu. Omba sana msamaha kwa Mwenyezi Mungu.
 
No sijamaanisha hivo. Nimenukuu mstari kwenye bible..ambao unaonyesha vitu ambavyo vinaweza kumshusha heshima mtu ni umalaya na ulevi.
Bado sijaamini hiyo stori ya kunywa pombe kua ndio imepelekea kufa kwake
Hata umaskini nao unashusha heshima mno mno..uandhalilika unajiona..basi tu..sio pombe na ngono tu
 
Mtangazaji wa kituo cha ITV cha jijini DAR ES SALAAM Bi Blandina Sembu amekutwa akiwa ameuawa maeneo ya ITV Mwenge usiku saa sita.

Mwili huo ulitambuliwa na Henry Mabumo aliyekuwa mtangazaji mwenzake kabla Mabumo hajahamia TBC.

Mwili ulichukuliwa na Polisi usiku huohuo.
Taarifa rasmi zitafuata.

=====

Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limethibitisha taarifa za kifo cha mtangazaji wa ITV Blandina Sembu, likieleza kuwa ni tukio la mauaji.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Ramadhan Kingai ameeleza kuwa walipata taarifa za mwili wa Blandina kutupwa mbele ya baa ya Maryland saa tano usiku.

Amesema gari aina ya Toyota Noah ilifika katika eneo hilo na kusimama kwa muda mfupi kabla ya kutupa mwili wa Blandina akiwa tayari amefariki.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa bodaboda waliokuwa wamepaki jirani na eneo hilo walishuhudia gari lililowashaa taa likisimama kwa dakika mbili kisha wakaona mwanamke ametupwa.

“Uchunguzi unaendelea ila tulichobaini huyu mtu hakuuliwa pale, mauaji yalifanyika sehemu nyingine pale walienda kumtupa.

“Amekutwa na majeraha usoni yanayoashiria alikuwa akijaribu kupambana kujitetea na hata jicho lake linaonekana alipigwa na kitu kizito,” amesema.

Kamanda huyo ameeleza kuwa makachero wa jeshi hilo wanaendelea na uchunguzi na muda si mrefu watawafikia waliotekeleza mauaji hayo.
Dah binafamu

RIP

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limethibitisha taarifa za kifo cha mtangazaji wa ITV Blandina Sembu, likieleza kuwa ni tukio la mauaji.

kifo-pcc-data.jpeg

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Ramadhan Kingai ameeleza kuwa walipata taarifa za mwili wa Blandina kutupwa mbele ya baa ya Maryland saa tano usiku.

Amesema gari aina ya Toyota Noah ilifika katika eneo hilo na kusimama kwa muda mfupi kabla ya kutupa mwili wa Blandina akiwa tayari amefariki.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa bodaboda waliokuwa wamepaki jirani na eneo hilo walishuhudia gari lililowashaa taa likisimama kwa dakika mbili kisha wakaona mwanamke ametupwa.

“Uchunguzi unaendelea ila tulichobaini huyu mtu hakuuliwa pale, mauaji yalifanyika sehemu nyingine pale walienda kumtupa.

“Amekutwa na majeraha usoni yanayoashiria alikuwa akijaribu kupambana kujitetea na hata jicho lake linaonekana alipigwa na kitu kizito,” amesema.

Kamanda huyo ameeleza kuwa makachero wa jeshi hilo wanaendelea na uchunguzi na muda si mrefu watawafikia waliotekeleza mauaji hayo.
 
Upande wetu ngono na pombe havitengamani ndio maana ma barmaid wanasavaiv na mshahara wa 40k.
Hasa konyagi....haina maana kabisa
Kwa wanaume huenda ni sawa wengine wakunywa hawapend kbs sex ...sijaiona kwangu tu ..nimekutana na wengi unataja tu upate vibe basu..sema kila mtu anaweza akaiendesha anavyotaka....
 
Kwa kutazama tukio tu, kauwawa kwingine na katupwa karibu na kazini kwake, Maryland bar , bar inayotumiwa na waandishi wa habari.
Aliemuua binti alitaka mwili uonekane kirahisi.
Vile vile mwuaji ana ujasiri alijua anafanya nini.

Kwa hiyo, aidha muuaji alipewa tenda ya kuua( ni proffessional) au kuna kitu bibie alikuwa anafahamu na kaondolewa uhai ili iwe onyo,
Au, bibie kuna watu amewazika katika dili.

Polisi huwa ni makini lazima hili wata liburumbua.
Hii ishu ina pande kama 3 hivi.
1.Kuna deal muhimu ambalo limekamilishwa ila mgao haukuwa mzuri. Aidha amewazidi kete wenzake.

2.Kuna taarifa ya muhimu sana anayo na wanajua yeye sio mtu mwenye koromeo. Angeenda kuripoti tukio hilo na kuleta madhara makubwa kwa jamaa flani.

3.Mahusiano ya kimapenzi, huenda amekula hela za mtu muda mrefu kisha akamletea mambo ya kingese na dhereu.
 
Back
Top Bottom