Dar: Mwandishi Bollen Ngetti adaiwa kutekwa tena na watu wasiojulikana; apatikana

Dar: Mwandishi Bollen Ngetti adaiwa kutekwa tena na watu wasiojulikana; apatikana

Nimeona hii habari nikabaki nashangaa.

Kupitia twitter,mtu anaejiita Martini M.M kapost hii habari tangu saa 11:28 alfajiri ya leo ila nashangaa sijui watu hawakuiona hii tweet maana reaction ni kama haikuwepo kabisa jambo linaloshangaza sana.

Hivi sasa inaonekane ame-post tena kama dakika 29 hivi zilizopita ila ukiifungua hiyo tweet inaonekana ni ya leo saa 11:28 alfajiri.

Anyway,labda tatizo ni mfumo wa masaa unaotumika ndio unaleta huu mkanganyiko.
Naomba kukufolo kule twita, hivi unaitwa nani vileeee!!!!
 
Andika kwa Lugha ya hoja na si matusi. Kwa nini kutukana kudhalilisha na kuvunja heshima ya mtu. Pinga kwa hoja utaeleweka
I am calling a Spade a Spade and not a big spoon. Kuwateka then kuwatesa na kuwaumiza wale wanaokupinga ni ushamba na upumbavu.
 
Huu uzi ni ushahidi tosha Watanzania wanaogopa Serikali. Hata Mbowe kesho akiminywa watu wataishi kupiga kelele tu lakini site hutaona mtu.
 
Capitano,

Kama polisi wanakiri wamemkamata kwanini unatoa taarifa kuwa ametekwa? Polisi kupitia makamanda wao wamekupatieni taarifa kuwa wako nae na wamemkamata si muende kuwauliza sababu ni zipi? kwa nini wanakamata watu kwa mtindo huo? Polisi watakuwa na sababu ya kumkamata kwa mtindo huo ambao mimi na wewe hatujui, lakini aliyekamatwa pengine anajua, sasa msitoe taarifa fake kwa kutafuta njia ya kueneza au to have political score.

Mimi sikubaliani sana na mambo mengi tu ya serikali au polisi au mkuu wa mkoa wa Dar, lakini siwezi pia kuwahusisha na matukio yanatokea Tanzania bila kuwa na ushahidi wa kutosha, lets calm tusikilize polisi wanasema nini, tunaweza tukapata haki zetu au kuitoa serikali iliyopo madarakani kwa njia sahihi tu sio kuvizia vizia matukio, like serious?

Mtu anakamtwa na serikali tunasema katekwa serikali, au mtu kweli katekwa na watu ambao hawajulikani tunasema polisi au serikali, je kama kuna uhalifu huu nchini tutalishughulikia vipi hili tatizo kama tutajikita kwenye political muda wote? kuteka haiwezi kuwa agenda ya kutupeleka ikulu, agenda should be Police reform, public security reform, sio huu utoto wa Instagram .
 
Wo shi niubi,
Ni polisi tu ndo wanaosema kakamatwa ila wananchi kwa uhakika kabisa tunajua katekwa na polisi. Na kuhusu kuwaamini hawa jamaa mmmh ni mashaka matupu kwasababu sinema ya unayoyaona leo hayajaanza jana wala leo na haya sio matukio ya kwanza tangu hata kabla ya akina Ulimboka.

Polisi wetu kwakweli ni wahalifu
 
Dah!..nini tena hiki? Sheria zetu zinaruhusu haya?
 
Roho ya shetani wewe ni shetani halisi
Hapana ndugu. Hata Mungu akiwatupa waovu motoni utasema ana Roho ya shetani. Swala lipo wazi kwanini kutumia lugha ya matusi kudhalilisha uzushi na kukuza maneno halafu usishughulikiwe.
 
Hapana ndugu. Hata Mungu akiwatupa waovu motoni utasema ana Roho ya shetani. Swala lipo wazi kwanini kutumia lugha ya matusi kudhalilisha uzushi na kukuza maneno halafu usishughulikiwe.
Mahakama c zipo kwann nishuhulikiwe kijambazi
 
Back
Top Bottom