Dar: Mwandishi Bollen Ngetti adaiwa kutekwa tena na watu wasiojulikana; apatikana

Dar: Mwandishi Bollen Ngetti adaiwa kutekwa tena na watu wasiojulikana; apatikana

Mtu anatekwa kisha anapata muda wa kumjulisha mke au ndugu kuwa katekwa na sababu anatoa, sasa hapo anakuwa katekwa au kajiteka, mtekaji anayekuruhusu ufanye mawasiliano huyo ni mtekani au mshikaji tu? Tuwe serious basi, hiyo itakuwa ni movie ya van dame.
 
Nimeona hii habari nikabaki nashangaa.

Kupitia twitter,mtu anaejiita Martini M.M kapost hii habari tangu saa 11:28 alfajiri ya leo ila nashangaa sijui watu hawakuiona hii tweet maana reaction ni kama haikuwepo kabisa jambo linaloshangaza sana.

Hivi sasa inaonekane ame-post tena kama dakika 29 hivi zilizopita ila ukiifungua hiyo tweet inaonekana ni ya leo saa 11:28 alfajiri.

Anyway,labda tatizo ni mfumo wa masaa unaotumika ndio unaleta huu mkanganyiko.
Kuwa hiyo Mkuu Salary Slip unahafiki Jeshi la Polisi kufanzia kazi taarifa/tetesi za mitandaoni?
Je unahafiki waanzishaji wa taarifa mitandaoni kuwa kama sehemu ya ushaidi?
 
Kama nchi imemshinda jiwe ajiuzulu tu. Hatutaki upuuzi wake wa kutulazimishia machafuko anaotuletea.
 
Waandishi Tunashukuru kwa kutupatia taarifa siku zote,lakini kuna baadhi ya taarifa mnazitoa kwa Mihemuko mikubwa sana, unapotoa taarifa ukihusisha serikali na utekaji unakuwa uko sahihi kweli? au unatoa taarifa ukihusisha na jambo lililopita huo ndio ushahidi kweli? Tatizo kubwa ni waandishi Mmejihusisha sana na siasa ndio maana makala zenu inakuwa ngumu Kuzichukulia maanani, umewahi kujiuliza serikali iteke raia wake kwa sababu zipi wakati huo inaweza Kumuita au Kumkamata raia yeyote kama kafanya kosa? tunaweza kuwa na aina mpya ya ugaidi au uharamia nchini ,badala ya kujadili swala hili kwa kina kwa nini linatokea hili swala mara kwa mara , kwa nini wakati huu, nini madhara yake kijamii na kiuchumi ,serikali ifanye nini, sisi Tunakimbilia kusema ni fulani au serikali, gues work will not take us any where, tujadili suala hili kwa kina bila kuvaa koti la uanaharakati au Wanasiasa.
Kwani wewe uko msumbiji?
 
Tulisema kuanzia mwanzo kabisa baada ya kulazimisha ushindi,kwamba kwa Magufuli huyu na chama chake,genge la maharamia linaenda kuweka mizizi.

Watanzania wakati tukiendelea kupiga kelele wengine walisema haya ni ya wapinzani hayatuhusu,vyombo vya habari vikaandamwa tukasema Mimi sio mwandishi....hali hii imeendelea kumgusa kila mwananchi...

Solution: Tukatae kwa pamoja hususan tusionufaika na genge hili la Maharamia,tuitumie falsafa ya nguvu na mamlaka yanatokana na umma.

Tukichelewa JPM atazidi kujiimarisha na kumuondoa itakuwa ngumu na itatigharimu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
JPM amechaguliwa kihalali . Kama una ubavu toka nyuma ya keyboard upinge nenda hata mahakamani basi. Tunampenda raisi wetu
 
Kutekana tena kwa wale wanaoandika usiyoyapenda wewe ni ushamba na upumbavu. Haya mambo ya kijima sana
Andika kwa Lugha ya hoja na si matusi. Kwa nini kutukana kudhalilisha na kuvunja heshima ya mtu. Pinga kwa hoja utaeleweka
 
Watz tuna maneno mengi vitendo zero. Haya mambo tulitakiwa kuyakataa tokea zamani siyo sasa. Watu kama tundu lissu walipigwa lisasi zaidi ya 30. Tena ndani ya sensitive government areas, watu kimya. Watu wamepotea, wamepigwa lisasi hadharani kama mwangosi na akwilina watu kimya. Leo hii tumejificha nyuma ya id fake tunapekecha maneno yasiyo na tija. Bora tukubali wajanja waendelee kufanya watakayo, tukubali hatuna uwezo wa kufanya chochote hivy tuache kelele.
 
Leo wananchi wenye kazi ya kusifu na kuabudu na kutetea kazi zote huyu muumiani mbona wako kimya sana
 
Wo shi niubi,
Uwana harakati au siasa ni huo wa kuhoji mantiki ya serikali kuteka raia wakati watu wameshuhudia na report inasema alikuwa kwenye bodaboda na akavamiwa na wahuni waliokuwa kwenye harrier na mkubwa wa polisi akasema hawakumteka ila walimkamata.

Sisi tunaona walimteka na polisi wanaona walimkamata. Lakini ajabu uko wapi? wakati polisi wetu wanaweza kusema risasi iliyomuua Aquilina ilipigwa juu na ikapinda kona na kumpiga marehemu yaani waliyasema haya mchana kweupeee. Labda ile senema ya sisitivi na picha zile imesahaulika.

Kama mtu ni Mtanzania kweli na ukafa ukaenda mbinguni na ukamkuta polisi mmoja tu wa kibongo huko, aisee toka mbio sana utakuwa umekosea geti la kuingilia
 
Hivi inawezekana vipi atekwe halafu haohao watekaji wamruhusu mateka wao afanye mawasiliano na mke wake.
 
Au ndo wanapelekwa kwenye lile jumba alilosema rafiki yetu Britanicca. Utawala huu utekaji umekuwa kama kazi ya malipo na marupurupu ni kama vile kuna reward ukiteka unapewa zawadi nono...Teka upate fedha.

Utekaji huu unalichafua Taifa SANA tena katika utawala huu ...kinachoumiza ni tuliemkabidhi Nchi hajawahi kutoka hadharani akalikemia lakini nakumbuka kuna mwana CCM Mwanza aliuwawa na wananchi akaagiza mara moja wahusika kukamatwa ...Rais wetu jitokeze ukemee utekaji huo kama Kikwete alivyokuwa anakemea ujambazi kipindi chake ..
 
Hivi inawezekana vipi atekwe halafu haohao watekaji wamruhusu mateka wao afanye mawasiliano na mke wake.
Kama upo kwenye gari yako binafsi na umeona NISSAN NYEUPE ...zinaweka roadblock ...na unajua real situation kwamba hawa ni wale unkown person lazima tu wanataka kufanya kidnapping ... muda huo unajua uliwahi kufuatiliwa huko nyuma kwa nini usifanye mawasiliano na mtu wako wa karibu...kwa kuhofia usalama wako..
 
Back
Top Bottom