Wakazi wa mtaa wa Kabaga Kinyerezi yamewakuta.
Ilikuwa ana kwa ana na panya road usiku wa manane. Kwa takribani masaa 2 ikivunjwa nyumba moja baada ya nyingine. Wakazi hao macho pima walikuwa wakichungulia madirishani, wakiwa wameufyata vilivyo mmoja baada mwingine akisubiria zamu yake.
Tutaamka lini sisi kutambua umoja ni nguvu wenye kuweza kutuokoa na yote?
Kwa hakika ni ujinga uliopitiliza kushindwa kuijua nguvu hii yenye uwezo wa kutuhakikishia haki zetu zinaheshimiwa na wote wanaojaribu kutupora.
"Mwenyekiti wa mtaa huo, Hashimu Gulana amesikitishwa na tukio hilo huku akiwalaumu wananchi wa mtaa huo kushindwa kupigiana simu kuwadhibiti vijana hao waliodumu kwenye eneo hilo kwa saa mbili wakitekeleza vitendo hivyo."
"Baada ya tukio, Polisi walikuja, lakini naomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa sababu hata tukio linatokea walikuwa wanachungulia madirishani badala wapigiane simu kuwadhibiti vijana hao," amesema.
Yale yale ya kumtaka mwingine kutupigania. Tutanyanyaswa hadi lini hata na vi-dogo vya miaka 12?
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.