Dar: Panya road wavamia nyumba 24, wanne wajeruhiwa

Nini tofauti ya wakazi wa kinyerezi madirishani na sisi na rojo la hawa waungwana wenye kututwisha tozo na maswahiba kibao kila uchao?
Siioni tofauti, kwasababu wao ni sehemu ya hii jamii tuliyopo, hapo wanatuwakilisha tu kwenye angle tofauti, huku bado tukiwa pamoja kwenye tozo.
 
Kauli ya mkt inatafsiriwa vibaya.

Nashauri atoke tena Kutoa ufafanuzi.
Mbowe kawapumulia kisogoni hao vijana, kawadhalilisha na kuwadharau BAVICHA lakini wanakenua na siku zote tunasema Mbowe kawaroga BAVICHA.

Mwenyekiti anawadharau wasio na magari ya milioni 400-500 na huku tunajua utajiri wa Mbowe umetokana na siasa ruzuku za CHADEMA.
 
Kwaiyo Kamanda Kasusa.......!

Wanapomsusa kwenye chaguzi Asianze kusingizia kaibiwa Kura....!

Tit for Tat.....!

Kura zinapigwa Kenya, huku rais ndio anaamua nani atangazwe mshindi na sio box la kura.
 
Tafakari ya kijinga iliyojaa upumbavu na ushamba kwa sababu tu hutaki CHADEMA nchini.
 

Tanzania hakuna tofauti kati ya mwenye degree na yule ambaye hajui kusoma. Toa mfano mwingine lakini sio wa degree.
 
Tunataka pepo kufa hatutaki🙄🤪
 
Mwenyekiti wa mtaa huo, Hashimu Gulana amesikitishwa na tukio hilo huku akiwalaumu wananchi wa mtaa huo kushindwa kupigiana simu kuwadhibiti vijana hao waliodumu kwenye eneo hilo kwa saa mbili wakitekeleza vitendo hivyo."
Kama wameamua kuishi kama makondoo waacheni
 
Mbowe alikuwa mmiliki wa Club Bilcanas akiirithi iliyokuwa Mbowe Hotels na aliajiri wafanyakazi wengi wakiwemo ma Dj
Kusema alikuwa DJ ni kuonyesha ukariri wa kikasuku
Umewahi kujiuliza kwa nini hayati Magufuli alihangaika kuivunja club hiyo?
 
Wanaume wa Dar!!!
 
Kura zinapigwa Kenya, huku rais ndio anaamua nani atangazwe mshindi na sio box la kura.
Makamanda mnajua kuruka ruka kama kuku walemavu. Tatizo lenu ni kutaka kuona time ya taifa ya uchaguzi inatangaza watu wenu kuwa washindi hata kama wameshindwa.

Kuna siku mwanachama wa CHADEMA alikuwa anasema Lissu ndiye aliyeshinda uchaguzi mkuu wa 2020 ila Magufuli ndio akatangazwa, nilicheka Sana kwa kuona hajui asemalo.

Nilimpa Elimu hii na pengine na wewe unaweza ukajifunza kitu.Elimu niliyompa ni juu ya mchakato mzima wa uchaguzi ambayo mimi niliugawa mchakato huo katika makundi matatu.

Kundi la kwanza: mchakato wa kupiga kura, katika mchakato huu wapiga kura wanapiga kura kwa kutumia karatasi ambazo zimekubaliwa na kuidhinishwa na vyama vyote na katika kituo Cha kupiga kura kila mpigakura anapewa karatasi moja tu na kabla ya kupiga kura kila msimamizi kutoka vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi anajiridhisha kwa kukagua masanduku ya kupigia kura. Baada ya hapo kura zinapigwa chini ya usimamizi na uangalizi wa karibu.

Kundi la pili, mchakato wa kuhesabu kura. Na hapa umakini uwepo maana ndipo panapolalamikiwa bila ushahidi. Naongea haya kutokana na experience ya uchaguzi mkuu wa 2020 katika uchaguzi ule utaratibu maalumu kabisa kwa kuhesabu kura ulitumika. Kila karatasi ya kura ilifunguliwa na ikapitishwa kwa makarani wa vyama kuikagua na kila mtu aliporidhika kura hiyo inahesabiwa kwa mhusika.

Kundi la tatu, mchakato wa kutangaza matokeo. Baada ya vyama vyote vilivyoshiriki kujiridhisha na zoezi zima basi matokeo yanatangazwa. Na mchakato huu pekee vyama vya upinzani huupinga.

Nini kinafanya upinzani usiridhike na matokeo? Vyama vya upinzani vinashindwa kuwa na maandalizi mazuri kuelekeo uchaguzi mkuu .

IEBC ya Kenya imeandaa uchaguzi uleule unaoandiliwa na NEC ya Tanzania kwa vigezo vilevile lakini aibu naona mimi mpinzani kushindwa kuona Hilo. Siku zote matokeo ya uchaguzi yanaumiza Sana ndio maana licha ya mahakama ya juu kubatilisha mapingamizi ya Odinga bado Odinga anasema haridhishwi na uamuzi huo hii inaonesha ni kiasi gani mpinzani yupo tayari kupinga matokeo hata kama alishindwa
 
Hawa polishi wameendelea kukaba za kupiga kiwi barabarani na kuacha ulinzi wa raia na mali zao ukizorota, wamebaki kumnanga Kinana baada ya kuwaambia ukweli....
 
Mtaa mzima walikuwa hawana vocha kuwataarifu polisi??
Hata kama walitaarifu lakini muhimu kutambua waliendelea kuchungulia madirishani nyumba moja moja ilivushwa kwa masaa 2.

Huo ndiyo utanzania sasa. Au siyo? Ujasiri wa kujipigania haupo hafi fulani atuiganie. Sisi wazuri wa kuelekea ilivyokuwa kama waandishi wa habari tu.
 
Comment Haina uhusiano na Uzi Huna akili.

Wananchi wamevamiwa na panya road wewe unaleta siasa za kipuuzi.
 

Kwamba?

"Kuna siku mwanachama wa CHADEMA alikuwa anasema Lissu ndiye aliyeshinda uchaguzi mkuu wa 2020 ila Magufuli ndio akatangazwa, nilicheka Sana kwa kuona hajui asemalo."

Kwani wewe ni yule mkurugenzi wa ile tume yetu pendwa?

Kwa mawazo yako CCM wanaweza kukubali kushiriki uchaguzi usiokuwa na tume au refa huru asiyekuwa wao?

Unajua kwa nini ASP Zenji hatimaye walifanya Mapinduzi au asili ya SMZ?

Kulikoni umbumbu huu?

cc: Zawadini
 
Mtajuta mwaka huu na mwigulu anawanyoosha bado , Burundi mtahamia Kwa lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…