Tatizo wauza madawa ya kulevya sio watu wachovu, ni watu wakubwa na wenye heshima kubwa kwenye jamii yetu. Yaani hata wakitajwa watu mtashika midomo kwa mshangao na kwasababu wanaheshimika sana hamta amini kama kweli ni wauza madawa badala yake mtaanza kuwatetea na kisha kumshambulia yule aliye wataja kuwa ndio mtu mbaya.
Wanaharakati wataibuka kila kona kisa tu katajwa fulani na hata Kama akikamatwa nayo bado watu watakuja tu nakusema kuwa kabambikiwa kwasababu ya chuki binafsi.
Wauza madawa ni hao hao wafanya biashara wakubwa ambao wakitajwa huto amini, wachungaji, mashekh, wasanii, wanasiasa wakubwa n.k
Utawaambia watu mchungaji wao ni muuza madawa nani atakuamini mfano ( ni mfano tu nisieleweke vibaya) umtaje Mtu Kama Mwamposa, Askofu Mwamakula n.k we unadhani waumini wake maelufu watakuamini kweli?
Umtaje MO eti anauza madawa nani atakusikiliza wana Simba wote watakuvamia kumbuka kilicho tokea kwa Manji.
Umtaje mwanasiasa Kama Zitto, Mbowe, Makamba, Nape n.k eti wanauza madawa weee hiyo kesi hutoiweza utapopolewa mawe nchi nzima hakuna atakae kuamini.
Ila ukweli unabaki kuwa ukweli kwamba hakuna mchovu mlalahoi wa tandale kwa mtogole mwenyewe uwezo wa kusafirisha madawa kutoka Colombia kuyaleta bongo hayupo. Wanao fanya hivyo ni watu wenye pesa zao, wafanya biashara, watumishi wa mungu tunao waamini, viongozi wakisiasa na wasanii wenye majina makubwa ambao ni vipenzi vya mamia ya watu.