Dar: Rais Samia awa Mgeni Rasmi Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

🤣🤣🤣🤣Huyu Hassan sina cha kumpa lakini Mungu ambariki sana
 
Mtetezi Mkuu wa Haki ni Katiba
Mtetezi Mkuu wa Haki hapa Nchini ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba hiyo ndio sheria mama, ina haki zote za wanadamu wanaoishi Tanzania, Swali langu, je, hao wanadamu tunaowatetea wanaijua hiyo katiba?
Kwa sababu hawaijui ndio maana tunataka makongamano ya Katiba.
 
Haki za kisiasa ndio zinajenga msingi wa haki zote. Hizo siasa ndio zina ratiba na kuweka misingi Mahakama na polisi wawe waadilifu kiasi gani.

Mama asitake kujificha kwa hili.

Mahakama imejaa wanasiasa wa ccm na humo polisi ndio usiseme. Haishangazi hata kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.

Hizi zote ni nguzo za vitendea kazi. Haki za kisiasa zinakuwa namba moja kwanza ndipo zinafata zingine.
 
Mama piga kazi tu
Hao wenye kupiga kelele ni wachache sana
Halafu ni wale walizoea kubebwabebwa na kulindwa lindwa
Mafanikio yanaonekana
Twende mbele
 
THRDC kukubali rais na serikali kwa jumla kushiriki ktk shughuli yao, wamekubali kung'olewa meno.
 
Ahsante kwa taarifa...

Kuna watu kadhaa nimewaona, including Founder wa JF...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…