DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Na ya Yona!
 
Nimeona sheikh anasema atashtaki JF kwamba wamemsingizia kuwa anafanya kampeni! Kiukweli ni vema na ingependeza zaidi kama angekaa akatulia maana sasa atapanic aanze kuongeza vitu ambavyo practically haviwezekani na akajitilia aibu bure!
 
Mange kasema atakula pilau la sheikh
Kwa hiyo sheikh ataondoka kabla ya mange
Hiviiii... kama asmaau ahlul badr inafanya kazi vizuri, kwanini netanyahu anadunda hadi sasa? Haya mambo mengine bwana yanafurahisha sana

Let's wait and see
 
Ime nuiwa hii
Haponi mtu
Kaaazi kweli kweli
 
Mimi naona mange angeachana na haya mambo Ya Dini na Imani kwa ujumla.
 
Siyo yy tu,sema yy anajiweka wazi ss tunajificha na matusi yetu,
Nafikiri wengi wetu hujibu kwa hisia but watukanaji matusi ya nguoni ni wachache.
Binafsi nikitukana huwa najiona mjinga wa mwisho. Utukanaji ni aina flani ujinga uliojichimbia chini sana na ambao hupunguza heshima.
Nafikri matusi tuwaachie makuli
 
Hyo shehe dhuluma tu... Hakuna dua itamkuta mtu hapo,, labda aroge sio DUA,,, kuna msikiti UPO MSAKUZI,, Kibamba,DAR.. , kawadhulumu waislam,,,

waislam WALIKUWA na ENEO Lao lakini hawana uwezo wa kujenga msikiti,,, jamaa kufuatwa akaleta wafadhili lakini pesa anapewa yeye kwnz,,akajenga msikiti tofauti na ramani ulivyo,, halafu akauhodhi,,,,

akaweka na shehe WAKE yeye,,, akapiga marufuku yeyote kujihusisha na uongozi wa hapo msikitini,,

matokeo yake waislam wameona bora wamsusie,, wakaenda kujenga msikiti mwingine,, na bado unasuasua kuisha,, yeye kabaki na msikiti ule na waumin 3 tu.... Hakuna mwislam wa eneo lile anayeswali pale msikitini....

AMEBAKI KUUTUMIA MSIKITI KUJIPATIA TENDE NA KANZU NA MISAADA MINGINE kutoka kwa wafadhili, Dhuluma sn huyo shehe,, asihusishe UISLAM na vitu vya KIPUUZI..
 
Sasa nikwambie, huyu jamaa licha ya kuwa shehe ila ni "mtoto wa mjini", ana "mbwa" mpaka marekani, jua hilo!
Kwa hyo mkuu jamaa ana changanya vitu viwili
Dini na utoto wa mjini na hao mbwa wake walioko marekani,
Basi hatari sana,kwa hyo siyo mbingu itayoamua Bali ni hao mbwa wake wa marekani?
Sidhani km umeongea sahihi,
Unamletea sifa mbaya kiongozi na waongozwa nae
 
mbona mzee wa upako alisema kuna waandishi kabla ya mwezi wa tatu watakuwa wamekufa ila mpaka leo wanadunda?
kuna kundi la viongozi wa dini nawafananisha na wanasiasa tu.......
 
hakuna ushahidi uliothibitika kuwa mtu aliyempiga lissu risasi anajulikana vinginevyo kama unamjua kawasaidie polisi itapendeza sanaa
Mkuu tumia akili kidogo,
Sijasema akamatwe maana hajulikani ila yupo,
Kukemea siyo kwa mtu anaeonekana maana anaeonekana akikosa anapaswa kukamatwa,kukemea huwa ni kulaani na kuonya kokote aliko muhusika ataskia ujumbe,
Mambo mangapi yanafanywa sirini na wanayakemea?
Hivi mpoje nyie!
 
Nadhaniii shehe apuuze tu huyu Dada afanye mishe zake kumijbu hyu Dada ni kumpa kiki ya hatariii mbona anatukan weng hawamjibuuuuu......atumie busara..!
Ndio ameshindwa kumpuuza.
 
Ghazwat ngoja nikae zangu hapa kwenye big screen (insta) tarehe 1 Jan 2019 nasubiri clip ya mdada Mange akifungua new year champaigne yake kusheherekea kuingia 2019 salama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…