DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

vyovyote vile... ndio maana kila mtu ana pata wasaa wa kumuomba yeye, hata kama ni mla rushwa, au nyongaji, muuaji... ndivyo inavyo kuwa... jiulize kwanini mapadre wanao najisi watoto mungu hawa angamizi hapo hapo...

mungu wetu ni mwenye huruma, upendo... nk... mungu alitaka kuwa angamiza wana wa israel lakini baadae musa alimuomba hasifanye hivyo na kupelekea kubadili maamuzi yake... rejea pale wana waisrael wakitoka utumwani misri
Na ya Yona!
 
Nimeona sheikh anasema atashtaki JF kwamba wamemsingizia kuwa anafanya kampeni! Kiukweli ni vema na ingependeza zaidi kama angekaa akatulia maana sasa atapanic aanze kuongeza vitu ambavyo practically haviwezekani na akajitilia aibu bure!
 
Mange kasema atakula pilau la sheikh
Kwa hiyo sheikh ataondoka kabla ya mange
Hiviiii... kama asmaau ahlul badr inafanya kazi vizuri, kwanini netanyahu anadunda hadi sasa? Haya mambo mengine bwana yanafurahisha sana

Let's wait and see
 
Inabidi ktk mahubiri na ushauri watoe neno msamaha watumie tu kisasi kwa kila jambo,
Hilo ndo fundisho wanalotupa,inamaana nikikorofiana na mke alonikosea na kuenda kwake kutaka ushauri basi nipewe hukumu na siyo kusamehe,
Sidhani km ametulia kabla ya kusema hili,Na nnawalaumu sana hao mashekhe walio pembeni yake,
Maana walipaswa kumshauri kwanza afundishe na kukataza na kuonya,huenda angebadirika,
Naamini kipo kilichowasukuma siyo bure
Ime nuiwa hii
Haponi mtu
Kaaazi kweli kweli
 
Mimi naona mange angeachana na haya mambo Ya Dini na Imani kwa ujumla.
 
Siyo yy tu,sema yy anajiweka wazi ss tunajificha na matusi yetu,
Nafikiri wengi wetu hujibu kwa hisia but watukanaji matusi ya nguoni ni wachache.
Binafsi nikitukana huwa najiona mjinga wa mwisho. Utukanaji ni aina flani ujinga uliojichimbia chini sana na ambao hupunguza heshima.
Nafikri matusi tuwaachie makuli
 
Hyo shehe dhuluma tu... Hakuna dua itamkuta mtu hapo,, labda aroge sio DUA,,, kuna msikiti UPO MSAKUZI,, Kibamba,DAR.. , kawadhulumu waislam,,,

waislam WALIKUWA na ENEO Lao lakini hawana uwezo wa kujenga msikiti,,, jamaa kufuatwa akaleta wafadhili lakini pesa anapewa yeye kwnz,,akajenga msikiti tofauti na ramani ulivyo,, halafu akauhodhi,,,,

akaweka na shehe WAKE yeye,,, akapiga marufuku yeyote kujihusisha na uongozi wa hapo msikitini,,

matokeo yake waislam wameona bora wamsusie,, wakaenda kujenga msikiti mwingine,, na bado unasuasua kuisha,, yeye kabaki na msikiti ule na waumin 3 tu.... Hakuna mwislam wa eneo lile anayeswali pale msikitini....

AMEBAKI KUUTUMIA MSIKITI KUJIPATIA TENDE NA KANZU NA MISAADA MINGINE kutoka kwa wafadhili, Dhuluma sn huyo shehe,, asihusishe UISLAM na vitu vya KIPUUZI..
 
Sasa nikwambie, huyu jamaa licha ya kuwa shehe ila ni "mtoto wa mjini", ana "mbwa" mpaka marekani, jua hilo!
Kwa hyo mkuu jamaa ana changanya vitu viwili
Dini na utoto wa mjini na hao mbwa wake walioko marekani,
Basi hatari sana,kwa hyo siyo mbingu itayoamua Bali ni hao mbwa wake wa marekani?
Sidhani km umeongea sahihi,
Unamletea sifa mbaya kiongozi na waongozwa nae
 
mbona mzee wa upako alisema kuna waandishi kabla ya mwezi wa tatu watakuwa wamekufa ila mpaka leo wanadunda?
kuna kundi la viongozi wa dini nawafananisha na wanasiasa tu.......
 
hakuna ushahidi uliothibitika kuwa mtu aliyempiga lissu risasi anajulikana vinginevyo kama unamjua kawasaidie polisi itapendeza sanaa
Mkuu tumia akili kidogo,
Sijasema akamatwe maana hajulikani ila yupo,
Kukemea siyo kwa mtu anaeonekana maana anaeonekana akikosa anapaswa kukamatwa,kukemea huwa ni kulaani na kuonya kokote aliko muhusika ataskia ujumbe,
Mambo mangapi yanafanywa sirini na wanayakemea?
Hivi mpoje nyie!
 
Nadhaniii shehe apuuze tu huyu Dada afanye mishe zake kumijbu hyu Dada ni kumpa kiki ya hatariii mbona anatukan weng hawamjibuuuuu......atumie busara..!
Ndio ameshindwa kumpuuza.
 
Ghazwat ngoja nikae zangu hapa kwenye big screen (insta) tarehe 1 Jan 2019 nasubiri clip ya mdada Mange akifungua new year champaigne yake kusheherekea kuingia 2019 salama!
 
Back
Top Bottom