DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Kweli kabisa hizi albadili kama zinafanya kazi huwafuata waswahili tu bhana maana Israel inawatendaje Palestina na hao hao Palestina wanaisoma namba?
Haiendi hivyo
Kila kitu kina 40 yake
Panga maisha yako yawe ya kistaarabu
Hivi unajua makafara wangapi wazungu au wahindi huwa wanatoa kumilki kitu chochote?
Hivi vitu vya Ulimwengu wa Roho si vya kupuuzia hata kidogo!
Kuwa mtu mwenye maadili mazuri na utakula mema ya nchi!
 
Aisee..kama mambo yanasemwa insta...dhidi ya huyu shekhe bac kuna tatizo kubwa sana.....
Hivi ndugu zetu waislamu nyie hayo mambo yaliyowekwa wazi huko inst dhidi ya huyu kiongozi wenu mlikua hamjui au??Manake ni kufuru tupu kwa kiongozi wa dini tena miongoni mwa dini zenye wafuasi wengi kuwa na kashfa nzito kama zile..watu wanatiririka tu kule.....
Bwakata waanzishe uchunguzi juu ya huyu jamaa...anawachafua sana waislamu....kiongozi mkubwa kama yule na yale makashfa bora angejiudhuru akaenda annual retreat hata Muscat huko.....
Zamani niliamini waislamu ni watu ambao hawataki mchezo hasa katika masuala yao ya dini..lkn kwa kashfa hizi za huyu jamaa....jinsi watu wanavyomlalamikia na bila shaka mlikua mnajua .....
Sheikh alijua kwamba watu wataendelea kumpaka matope, na akasema hatajibishana naye tena!
Sasa hao wengine ni kufurahisha baraza tu!
NENO LAKE AMESHA LITAMKA
MWENYE MASIKIO NA HEKIMA AYASIKIE!
 
Kwa sentensi chache niseme nionavyo mimi kuhusu hii "vita mpya" kati ya dada Mange na Sheikh mkuu Dar, Alhad Mussa Salum. Kwanza nieleze tu kuwa nauheshimu sana Uislamu kama navyoheshimu imani za watu wengine. Pia nawaheshimu viongozi wa kiislamu wakiwemo masheikh kama navyoheshimu viongozi wa imani na madhehebu mengine.

Lakini nadhani Sheikh Salum hakuwa na sababu ya kumjibu Mange. Kuna mambo ambayo tunategemea kuona Sheikh Mkuu wa mkoa akifanya, sio kufuatilia mambo ya instagram na kujibu. Tunategemea kuona akipambana kupigania haki za waislamu ktk namna itakayoleta matokeo chanya kwa waislamu na taifa kwa ujumla.

Tunategemea kumuona akiwasemea masheikh waliokamatwa miaka zaidi ya mitano iliyopita na mpaka leo wapo tu mahabusu bila kujua hatma yao. Aombe kesi zao zisikilizwe haraka (JPM anasema chapchap) ili kama wana hatia wahukumiwe, na kama hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani basi waachiwe HURU, kuliko kuendelea kuteseka tu mahabusu miaka zaidi ya mitano kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.

Hivi wakikaa mahabusu miaka 10 halafu bado ushahidi wa kuwatia hatiani usipatikane itakuaje? Au wakakaa mahabusu miaka 30 halafu wakaja kuachiwa huru kwa kuonekana hawana hatia itakuaje? Sheikh Salum haoni kama wenzake watakua wameteseka bila sababu? Sasa kwanini asiwasemee? Wanasheria wanasema "Justice delayed is justice denied", yani haki inayocheleweshwa ni haki iliyopotezwa.

Hawa masheikh wakiendelea kukaa mahabusu kwa miaka mingine zaidi na wakaja kukosekana na hatia it is justice denied. Ndio maana nilimpongeza Rais JPM alipomwambia Jaji Mkuu kwamba anapenda kuona kesi zikisikilizwa chapchap. Naamini na hii ya Masheikh itasikilizwa "chapchap" kama alivyoshauri Rais JPM (japo wameshasota miaka mingi sana ndani).

Je Sheikh Salum anajua kuna wenzie wanaoteseka huko magerezani? Wapo wanaodaiwa kudhoofika sana kiafya, wakiwemo akina Sheikh Fareed, Mselem na wengine. Nilitegemea kuona Sheikh Salum akipambana kwa ajili ya HAKI na USAWA kwa watanzania wote (wakiwemo masheikh walioko gerezani) na sio kupambana na Mange Kimambi. I stand to be corrected.!!

Malisa GJ
Nadhani lengo la mtoa uzi,ni kuhusu masheikh waloko rumande.sasa unataka sheikh aingilie mahakama au aipaingie mahakama nn cha kufanya.
 
Duh;
Naona kama vile Yule Sheikh wetu anamwambia Da Mange Please Hide my ID.

Hivi lakini mbona naona kama kuna mambo fulani hayako sawa kwa huyu sheikh.Sasa kweli anataka Da Mange amtetee kweli?Au anatafuta kiki kwa pikipiki au kuna mambo mengine anaogopa tusijiue

Anyway

Da Mange Please Hide My ID

Pole Alhaji

Usijali ndio maisha yalivo
 
Aisee..kama mambo yanasemwa insta...dhidi ya huyu shekhe bac kuna tatizo kubwa sana.....
Hivi ndugu zetu waislamu nyie hayo mambo yaliyowekwa wazi huko inst dhidi ya huyu kiongozi wenu mlikua hamjui au??Manake ni kufuru tupu kwa kiongozi wa dini tena miongoni mwa dini zenye wafuasi wengi kuwa na kashfa nzito kama zile..watu wanatiririka tu kule.....
Bwakata waanzishe uchunguzi juu ya huyu jamaa...anawachafua sana waislamu....kiongozi mkubwa kama yule na yale makashfa bora angejiudhuru akaenda annual retreat hata Muscat huko.....
Zamani niliamini waislamu ni watu ambao hawataki mchezo hasa katika masuala yao ya dini..lkn kwa kashfa hizi za huyu jamaa....jinsi watu wanavyomlalamikia na bila shaka mlikua mnajua .....
BAKWATA department ya CCM hatuitambui. Viongozi wanaotambuliwa na kuheshimika Sheikh Issa Ponda, Masheikh wa UAMSHO.
 
Amsema ni mwaka wake wa mwisho wanaenda kumuombea dua hata endelea na upuuz wake kwan ye nani
 
Aisee..kama mambo yanasemwa insta...dhidi ya huyu shekhe bac kuna tatizo kubwa sana.....
Hivi ndugu zetu waislamu nyie hayo mambo yaliyowekwa wazi huko inst dhidi ya huyu kiongozi wenu mlikua hamjui au??Manake ni kufuru tupu kwa kiongozi wa dini tena miongoni mwa dini zenye wafuasi wengi kuwa na kashfa nzito kama zile..watu wanatiririka tu kule.....
Bwakata waanzishe uchunguzi juu ya huyu jamaa...anawachafua sana waislamu....kiongozi mkubwa kama yule na yale makashfa bora angejiudhuru akaenda annual retreat hata Muscat huko.....
Zamani niliamini waislamu ni watu ambao hawataki mchezo hasa katika masuala yao ya dini..lkn kwa kashfa hizi za huyu jamaa....jinsi watu wanavyomlalamikia na bila shaka mlikua mnajua .....

Kaka labda nikupe elimu ambayo huijui tafadhal kuwa makini nisikilize.
BAKWATA sio chombo cha waislamu na haitawahi kuwa kwa sababu hakikuundwa na waislamu. Mfano mzur nikuulize tu, hivi inawezekana vipi wakristu muundiwe baraza na serikali tena inayojinasibu kwamba haina dini?

Hii kitu ina historia ndefu kidogo nyuma ktk vuguvugu la uhuru, ikumbukwe wakat wa kupigania uhuru baadhi ya wazee wengi wa DSM walihusika na ukomboz wa nchi yetu then kilichokuja kutokea ni kugeukana miongoni mwao baadae. Yaan hawakushirikishwa ktk matunda ya uhuru, ikumbukwe DSM ilikua na wazee wengi ambao ni waislam wakaanza kuonesha hasira zao kwa serikal ya Nyerere wakiona km amewageuka hawakumbuk tena ktk uongoz wake. Nyerere alichokifanya ni kitu simple tu "divide and rule" akawaundia BAKWATA akiwataka waislam ku-obey hcho chombo na serikali itacomply tu kile kiongeacho na BAKWATA. Hapo ndio utata ulipoanza, wengine wakakubal wngne wakakataa.

Hicho chombo kina mkono mkubwa wa serikal, km mfuatiliaji wa siasa za nchi hii utakubaliana na mm kwamba kiko pale kwa manufaa ya wachache na ndio maana muislam unayejielewa huwez kukubal kutawaliwa na BAKWATA. Wao kaz yao ni kutafuta aya na hadith znazowapa favour kwao ila co umma wa kiislamu.

Hivi BAKWATA ingekua chombo cha kiislam kingeshindwa walau kuhoji uhalali wa masheikh wa uamsho kuwa rumande hadi leo tena kwa kesi nyepesi namna ile?

Kwahyo ndugu yangu kuhusisha uislam na BAKWATA ni kutukosea bora tu utuache uizungumzie km tawi la CCM na shirika la serikali.
 
Sio kila mtu yupo ig ingependeza kama hayo matusi ya mange yangepandishwa hapa

Sheikh has stooped to a new low kujibizana na Mange
 
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.

Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, wajiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Anataka kumloga au ni vipi mazeee.... Maana huo mkwara sio...
 
Back
Top Bottom