DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Aisee hiyo kitu ipo kabisa na Mola huwa anasikia!
Nimeshuhudia watu wakianguka
Mtu mwenye ukaribu na Mwenye Enzi Mungu sio wa kuchezea
Soma kitabu cha Samueli
 
labda kama tuna imani tofauti... mungu anakupa kwa hitaji lako... hata ukitaka kuua...! au mpaka tukupe aya mkuu...! mungu sio wako pekee... ni wawote... wabaya, watakatifu... nk wanyama...
 
Kila mchuma janga hula na nduguze,juzi tumemzika jamaa kwa dhulma ya wizi...kaenda kuvamia kwa ndugu zetu wakigoma nao wakajibu mapigo Mara baada ya kutangaza kwa siku tatu mfululizo.RIP frank jembe langu.
Hii misemo mingine sio ya kupuuzia kwa kweli!
Si unakumbuka kesi ya kina Nyaga Mawala na wanawake wa kimasai?
Ehh Maulana Mola wangu tunusuru walahi!
 
Aliyemshauri kumjibu Mange ndio kakosea.. Pole sana kwa sheikh, ila Mange kamwambia ukweli mtupu... Mange ni mwana TANU yule, hivi mnazikumbuka ahadi kumi za mwana TANU? Basi Mange anaziishi zile ahadi zote hasa ile ahadi inayosema "8.Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko". Na kama kuna ahadi Mange imemshida kidogo ni moja tu ile ya mwisho... "10. Nitakuwa mtii kwa Raisi na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania". hiyo tu...
 
Lusekelo alimtaka Ney wa mitego hasi mjaribu mungu... kwa uhuni wake wa kutaka kuanzisha kanisa... bila uelewa mpana wa bible...
 
sifikirii na sidhani kama mange atadhurika

jambo la aibu sana kiongozi wa dini kumtamkia mfuasi ukomo kisa mna personal interest alitakiwa amsahihishe tu na kumsaidia kimawazo lakini suala la ukomo wa mtu hilo ni jambo la Mungu tena
 
Aisee hiyo kitu ipo kabisa na Mola huwa anasikia!
Nimeshuhudia watu wakianguka
Mtu mwenye ukaribu na Mwenye Enzi Mungu sio wa kuchezea
Soma kitabu cha Samueli

Hakuna mtu mwenye uwezo huo mkuu. Kinachoweza kutokea ni watu kumuvizia mhusika na kumuwekea sumu katika vyakula au mazingira ambayo akigusana nayo anadhurika taratibu au ghafla tu. Vinginevyo Mungu hawezi kusikiliza sala za kijinga za watu wake wafe kabla ya malengo ya watu hao kuumbwa butimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…