DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Mahakama ya mbinguni imetoa tamko la hukumu au yeye anatoa,afu kwanini asimpotezee ,inachukua mda gani mahakama kutoa hukumu,hiyo mahakama adhabu yke ni kifo tu?

Naona kifo ndio hukumu ya juu kabisa. Sasa hukumu za Vifo huwa zinakuwa-specified kabisa kama ni kunyongwa,kudungwa sindano au vinginevyo. Sasa muda ukikaribia Wa hiyo hukumu kutekelezwa tunamuomba arudi Idara ya Habari Maelezo atueleze hukumu hiyo itatekelezwa kwa njia gani. Asije akapata nguvu tu za kutueleza juu ya uwezekano Wa hukumu lakini akatokomea kutueleza juu ya aina ya hukumu ya kifo husika.

Kwanza huyo Sheikh amefanya kosa la Jinai. Alitakiwa akamatwe hapo hapo aelekezwe Central Police kwa mahojiano. Huwezi kutishia juu ya "kunyamazishwa" kwa MTU yeyote yule duniani ama awe RAIA Wa nchi au vinginevyo. Serikali ya nchi yetu haina dini na hivi huwezi kukusudia "kunyamazisha" watu kwa kisingizio cha Dini yako inakuelekeza hivyo!
 
Sijui Mamnge kimambi anashida gani, ni mdada asiye na Ustaarabu na Staha wala adabu. Anachofanya hakosoi kama wengi wetu wanavyomshabikia ila huwa anatukana tena matusi yasiofaa kabisa. Kwani hana njia nzuri ya kukosoa kweli? Ivi bungeni wangekuwa wanakosoa Serikali kwa staili hii ingekuwaje?; Kwa Clip nilivyoisikiliza na Shehe namna alivyozungumza; Ni wazi kuwa hakustaili kujibiwa kwa staili ya Mange; inshort sijaona kuna haja gani Mange kuachia matusi kwa Shehe?
 
Umeongea point sana
 
Shem avatar yako nzuri
hahahaha kama naiona ngoma ya yule jamaa [seduce me]
watanzania bhana wanapokea taarifa then wana take advantage humo na hizi ndio sosho netiweki.
note.cole williams na shunnie jukwaa lenu lipo tumewawekea jaribuni ku scroll down!!
 
Mh. Sheik Salum, Shehe wa Mkoa wa Dar Es Salaam, dini zinakosa kuaminika siku hizi kwa matamshi kama haya. Kama mwaka utaisha na Mange akaendelea kudunda (and this is most likely so) utakuja na story gani? Watu tunakuwa wepesi wa kusahau. Nakumbuka Scopioni alipomtoa macho masikini raia, watu walisema haya makanisa ya Lwakatale, Mzee wa Upako, Kakobe, Gwajima etc, waliombwa waende wafanye maombi ya miujiza yao raia apone. WOTE WALIINGIA MITINI MAANA WALIJUA KUWA HAWANA UWEZO WA KITU KAMA HICHO NA HAKIPO. HAKUNA SAYANSI YA HIVYO NI UONGO.
Sasa ikitokea hivyo utakuja na story gani? Ingelikuwa vizuri ukajimazia.
 
Sijui [Mamnge] kimambi anashida gani, ni mdada asiye na Ustaarabu na Staha. Anachofanya hakosoi ila ni kutukana. Kwani hana njia nzuri ya kukosoa kweli; Kwa Clip nilivyoisikiliza kuna haja gani Mange kuachia matusi kwa Shehe?
mkuu ulivushwa darasaa aisee maana errors za kutoshaa
SIO;Mamnge
NDIYO;Mange kimambi
 
Naaam na hapa ndo tunaona kilichopo ndani ya mioyo ya viongozi wetu wa dini
Ambao wanatufundisha msamaha lkn wao hawasamehi,wanatufunfisha kuepuka visasi lkn wao ndo mabingwa wa visasi,
Huu si mfano mzuri kabisa
Ndiyo maana nawaacha na dini zao. nitasali dini za babu zangu!
 
Ustadhi hakupaswa kumjibu hata mara moja.
angekaa kimya tu kwa kupotezea kama hakuna kilichotokea.
 
Reactions: Mdf
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…