DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

sifikirii na sidhani kama mange atadhurika

jambo la aibu sana kiongozi wa dini kumtamkia mfuasi ukomo kisa mna personal interest alitakiwa amsahihishe tu na kumsaidia kimawazo lakini suala la ukomo wa mtu hilo ni jambo la Mungu tena
Zingekuwa na nguvu wangedhurika wanajeshi wa marekani au waisrael kwa dhuluma wanazotenda middle east na Afghanistan,
 
Kupitia sheikh huyu Jamii forums inaweza ikatikiswa tena......naona wanataka kuua ndege wawili kwa jiwe moja.
 
Hicho anachokieleza kwamba Mange "ataondoka" ni kuwazia mambo yasiyowezekana! Katika nyakati zetu ni lazima kuacha kutumia matisho kama zamani kwamba ukimfanya hivi dhidi ya dini utadhurika. Kama anamaanisha kuwa Yeye Sheikh na viongozi wenzie watamuomba Mungu ili "amupumzishe" Kimange hilo ni jambo ambalo Mungu hawezi kufanya kabisa! Labda kama kuna Mungu tofauti na tunayemjua wengine. Ningeelewa zaidi ikiwa angemuombea Mange maisha marefu na kujaliwa moyo Wa kutambua makosa yake na kutubu.
Kutubu dhambi na kuziacha bila kuzirejea tena, ndiyo TOBA inayohubiriwa na madhehebu ya dini na watumishi, sio kuwamaliza wakati hawajatubu, huyo kiongozi kapitiliza sana. Ajabu.
 
Sheikh wa mkoa anachaguliwa au anateuliwa?! Mbona yeye tu, sheikh wa wilaya ni yupi?! Huyu uswalisha msikiti gani?! Ni msikiti upi ni wa mkoa?! Je, mikoa mingine wapo kama yeye au ni Dar tu?!
 
Kwani amesema atakufa au kasema kutukana mwisho mwaka huu?

Kwani mange akiacha kutukana ni vibaya sana? Kwanini tunataka aendelee kutukana viongozi wa dini?
Kasema hatutamsikia tena sasa tafsiri yake si Baba Jenny bye bye
 
Mahakama ya mbinguni imetoa tamko la hukumu au yeye anatoa,afu kwanini asimpotezee ,inachukua mda gani mahakama kutoa hukumu,hiyo mahakama adhabu yke ni kifo tu?
 
Naaam na hapa ndo tunaona kilichopo ndani ya mioyo ya viongozi wetu wa dini
Ambao wanatufundisha msamaha lkn wao hawasamehi,wanatufunfisha kuepuka visasi lkn wao ndo mabingwa wa visasi,
Huu si mfano mzuri kabisa

Ndio maana inafika mahali tunahoji Dogma za dini zingine. Kama issue ni matusi ya Mange kwa watu hajaanza Leo kutukana. Kwa nini huyo Sheikh hajawahi kumuomba Mungu "amupumuzishe" huyo Mange kwa matusi kwa watu wengine mbalimbali? Kwa hiyo,Sheikh anataka kutueleza kuwa Mungu "anaumwa" sana na matusi kwa Masheikh na Wachungaji kuliko raia Wa kawaida? Ina maana ndio kusema "masikio" ya Mungu yanapokea frequencies tofauti tofauti za matusi?
 
mjomba ukibishana na mpumbavu na wewe utakuwa hivyo hivyo sheikh angetumia busara zake kama kiongozi wa dini kuonyesha mfano kama kiongozi wa dini kwa wafuasi wake
lakini sio kwa kupovuka na vitisho
umetokea sura gani maalim?

Haitasaidia nikikwambia nimetokea sura gan,ya wap,na ya nani cha msingi ni wajibu wa kila mmoja wetu kukemea uovu unaojitokeza na utakaojitokeza katika jamii inayotuzunguka.

Shekhe amemzungumzia mange kutokana na vitendo vyake vya kuudhi,kebehi,kashfa na lugha chafu ambazo si stahiki kwa jamii yetu hii ya "hapa kazi tu"
binafsi naunga mkono tamko hili na pia ni wito kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea maovu yatakayojitokeza.

Huu ni mfano wa kuigwa.hakuna personal interest yeyote kama wengi wanavyodai.
Na
yeddy guyy
[Gemstone dealer]
 
Back
Top Bottom