DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Na yeye angevunga tu , hapo sasa ndio ataharibu, bora atumie muda huo kupiga dua ya kuliombea taifa. Dhidi ya watu wasio litakia mema taifa hili

Hicho anachokieleza kwamba Mange "ataondoka" ni kuwazia mambo yasiyowezekana! Katika nyakati zetu ni lazima kuacha kutumia matisho kama zamani kwamba ukimfanya hivi dhidi ya dini utadhurika. Kama anamaanisha kuwa Yeye Sheikh na viongozi wenzie watamuomba Mungu ili "amupumzishe" Kimange hilo ni jambo ambalo Mungu hawezi kufanya kabisa! Labda kama kuna Mungu tofauti na tunayemjua wengine. Ningeelewa zaidi ikiwa angemuombea Mange maisha marefu na kujaliwa moyo Wa kutambua makosa yake na kutubu.
 
Yaani Shekh angekaa kimya tu angejijengea heshima kubwa sana. Huyu kasemwa kidogo tu na kamtu kama Mange tena kwenye instragram kaita press conference na kutishia kuua je angesulubiwa kama Yesu angefanyaje?
Alipashwa amuombee kwa mwenyezi Mungu amrejeshe kwenye mstari na sio kumlaani,
Mtume alipigwa mawe na akawaombea waliompiga Mungu awasamehe, Yesu pia aliwaombea wakosaji wasamehewe
 
Lusekelo alitoa matamko kwa waandishi wa habari kuwa watakufa ila hadi leo hakuna aliyekufa mbaya sana naye mwenyewe hajaenda kuuza gongo kama alivyoahidi.

Shekhe naye kaingia mkenge ule ule wa Mzee shekhe Yahya,.

Yaani, daima siasa uchwara mbuzi zitakutokea puani tu ukijiingiza bila kufata principles.

Tunasubiria mwisho wa Mange kimambi ndani ya hii 2018.
Ila akivuka hadi 2019 sijui majibu yake kwa shekhe yatakuwa ni nini hasa!? Shekhe ajiandae kupata aibu za daima pale Miss. Kimambi atakapo toboa hadi 2019

Any way, Shekhe na hadhi yake kwa dini na hapo nchini siyo mtu wa kujibizana na Mangi Kimambi.
 
Back
Top Bottom