DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Kama kumchokonoa Mange tuu[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Yule ni hatari. Watu tuna makandokando mengi, hivyo kama unajitambua usimchokoze! particularly, kama ulivyosema if you are a highly placed person in the society!
 
Mbona hutaji Boko haram, Al kaida na al shabab hao wanayofanya ni halali? Je Yemen wanauawa na nani kama siyo waislam wenzao wa Saudia? Je, Taliban wanaowaua ndugu zao ni wamarekani? Albadili ya shekh amesema itatupata hata sisi member wa JF. Yeye ameingiaje kama siyo member basi na yeye tutakufa naye.
Pilau lake tutalila[emoji23] [emoji23] [emoji38]
 
Aisee hiyo kitu ipo kabisa na Mola huwa anasikia!
Nimeshuhudia watu wakianguka
Mtu mwenye ukaribu na Mwenye Enzi Mungu sio wa kuchezea
Soma kitabu cha Samueli
Kama ni kweli George Bush wote wawili wasingekuwa hai kwa walichokifanya Iraq.
 
Akuna kitu kama icho wewe watu wameua Osama,Gaddafi tena msikitin kuna wanaoijua din kama waharab walisomea misikiti Obama yule bado anadunda tuuh
Kweli kabisa hizi albadili kama zinafanya kazi huwafuata waswahili tu bhana maana Israel inawatendaje Palestina na hao hao Palestina wanaisoma namba?
 
Halafu huyo dada wa ma-mtoni ana wafuasi wengi hatari TZ na hasa hawa vijana wa 20-40 yrs,na mbaya sana wanamsikiliza na kuamini anachoongea.Ni hatari sana
 
IMG_20180206_071226_167.jpg
 
Tuhuma hubaki kuwa tuhuma mpaka pale itakapothibitika... Kinyume chake hugeuka kuwa uzushi..

Wachina wana taratibu zilizonyooka sana... Kitendo tu cha kutumiwa kinakulazimisha kuondoka kwenye wadhifa ama nafasi uliyonayo mpaka itakapothibitika vinginevyo... Kama tuhuma husika zilikuwa uzushi umewini na aliyekutuhumu inakula kwake.... Lakini kuna swali hubaki hewani... Kwanini utuhumiwe wewe?

Tuhuma humuondolea mtu heshima... Humuondolea mtu uaminifu na kuaminika... Hufedhehesha na kuleta aibu kwako na kwa jamii yako... Tuhuma za wizi rushwa na uasherati huwa na uzito wake tofauti kabisa na tuhuma nyinginezo kama uchawi nk...
Anapotuhumiwa mtu wa kawaida... Haiwi jambo kubwa sana kama anapotuhumiwa kiongozi wa kiserikali ama wa kisiasa au kijamii... Lakini pia tuhuma za kiongozi wa kijamii pia zinaweza zisibebe uzito sana kama tuhuma za kiongozi wa dini.. Na pengine kiongozi mkubwa wa dini...

Kiuhalisia na kijamii pia bila kusahau kiimani... Tuhuma si jambo jema, si jambo la kheri kabisa.. Hufedhehesha na kutia aibu... Muungwana ni kitendo... Mtu anapaswa kuonyesha uwajibikaji na kujali kwa kujiuzulu mpaka tuhuma zitakapothibitisha vinginevyo... Na hii ni kutaka kulinda heshima yako, ya familia yako na jamii nzima unayoiongoza... Kujiuzulu hakumaanishi kuwa ni kweli umetenda bali ni kutoa nafasi ili kupisha uchunguzi na kuepusha sononi kwa jamii yako... Yaani matendo ya tuhuma zako visihusishwe na cheo wala imani yako

Kuna kiongozi mkubwa wa dini (Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam) kashauriwa vibaya na pengine kwa kughafilika akasahau weledi.. Akasahau dhima na wajibu wake katika jamii... Akaitisha press conference kutoa vitisho ama unabii kuwa kuna binti mwanaharakati Mitandaoni maarufu kama Mange Kimambi huu ni mwaka wake wa mwisho kuishi kutokana na kuwatukana viongozi na watu mbalimbali... Nadhani akiwepo yeye

Hili halikukaa vizuri sana kwakuwa kisheria nj kwamba kiongozi wa dini ametoa kitisho cha dhahiri cha kuangamiza.. Yaani ametishia kuua... Hapa ndio Mange kapashikia bango.... Matamshi ni kama risasi ikitoka imeroka haina rivasi... Kiongozi hakupaswa kuyasema yale... Naamini kuna mfumo wa uongozi ndani ya taasisi anayoiongoza.. Walau angemwachia msemaji wa taasisi amjibu Mange kama kungekuwa na ulazima wa kufanya hivyo... Mgawanyo wa madaraka una maana kubwa sana.... Sasa hivi Mange akipatwa na baya kiongozi atashangilia unabii ila kutakuwa na ukakasi mwingi kwenye jamii.....

Press conference ya kupitisha hukumu ya kifo cha Mange imezua balaa kubwa... Mange hana dogo na hana cha kupoteza ila ana wafuasi wengi na wanaojua mengi pengine kuliko hata kiongozi husika.. Mange akalianzisha kwenye mtandao wake wa Instagram... Halafu wafuasi wake wakaanza kufunguka siri za kiongozi wa dini, kuanzia ulawiti, uasherati mpaka mambo ya aibu kabisa kama ya kufanya ngono kwenye gari na ofisini, kuhonga na kutembea na wake za watu... Watu wanatiririka hasa.. Huku ni zaidi ya kuvuliwa nguo...
Pengine kati ya hizo inawezekana nyingine ni tuhuma tu zisizo na chembe ya ukweli.. Lakini tayari kiongozi keshachafuliwa vibaya... Anadhalilika yeye familia na taasisi anayoiongoza... Tuhuma ni nyingi mno... Kila jambo hutokea kwa sababu... Je hili limetokea ili kiongozi wa dini mabaya yake yadhihirike?
Vyovyote iwavyo kuilinda taasisi, kuilinda familia na wanajamii wake.. Na kulinda heshima kidogo aliyobakiwa nayo.... ASHAURIWE KUPUMZIKA.....

Mshana kuna kitu inaitwa "Emotional Intelligence" baba!! Nikiangalia viongozi wetu, ni wachache sana wameweza kumudu hii kitu! Huyu shehe nguvu kubwa aliyotumia kumjibu Mange, bora angeenda kulala angelinda heshima yake zaidi. Kinachomuuma shehe huyu ni ukweli kujulikana, sasa kujibu kwake amemwaga petrol kwenye moto. Atatabiri vifo vya wangapi? Au yeye hatokufa? Haya mambo ya watu wengine kujifanya kuwa Mungu anawasikiliza wao zaidi ni kukengeuka aisee!!
 
Kama ni kweli George Bush wote wawili wasingekuwa hai kwa walichokifanya Iraq.
Sadamu naye alikuwa na makosa yake!
What goes around comes around
That is the law of Universes
Lazima uvune unayo yapanda hakuna kuepuka
 
Bora angenyamaza tumeanza kumjua shekhe kwa undani kabisa
 
Kwa sentensi chache niseme nionavyo mimi kuhusu hii "vita mpya" kati ya dada Mange na Sheikh mkuu Dar, Alhad Mussa Salum. Kwanza nieleze tu kuwa nauheshimu sana Uislamu kama navyoheshimu imani za watu wengine. Pia nawaheshimu viongozi wa kiislamu wakiwemo masheikh kama navyoheshimu viongozi wa imani na madhehebu mengine.

Lakini nadhani Sheikh Salum hakuwa na sababu ya kumjibu Mange. Kuna mambo ambayo tunategemea kuona Sheikh Mkuu wa mkoa akifanya, sio kufuatilia mambo ya instagram na kujibu. Tunategemea kuona akipambana kupigania haki za waislamu ktk namna itakayoleta matokeo chanya kwa waislamu na taifa kwa ujumla.

Tunategemea kumuona akiwasemea masheikh waliokamatwa miaka zaidi ya mitano iliyopita na mpaka leo wapo tu mahabusu bila kujua hatma yao. Aombe kesi zao zisikilizwe haraka (JPM anasema chapchap) ili kama wana hatia wahukumiwe, na kama hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani basi waachiwe HURU, kuliko kuendelea kuteseka tu mahabusu miaka zaidi ya mitano kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.

Hivi wakikaa mahabusu miaka 10 halafu bado ushahidi wa kuwatia hatiani usipatikane itakuaje? Au wakakaa mahabusu miaka 30 halafu wakaja kuachiwa huru kwa kuonekana hawana hatia itakuaje? Sheikh Salum haoni kama wenzake watakua wameteseka bila sababu? Sasa kwanini asiwasemee? Wanasheria wanasema "Justice delayed is justice denied", yani haki inayocheleweshwa ni haki iliyopotezwa.

Hawa masheikh wakiendelea kukaa mahabusu kwa miaka mingine zaidi na wakaja kukosekana na hatia it is justice denied. Ndio maana nilimpongeza Rais JPM alipomwambia Jaji Mkuu kwamba anapenda kuona kesi zikisikilizwa chapchap. Naamini na hii ya Masheikh itasikilizwa "chapchap" kama alivyoshauri Rais JPM (japo wameshasota miaka mingi sana ndani).

Je Sheikh Salum anajua kuna wenzie wanaoteseka huko magerezani? Wapo wanaodaiwa kudhoofika sana kiafya, wakiwemo akina Sheikh Fareed, Mselem na wengine. Nilitegemea kuona Sheikh Salum akipambana kwa ajili ya HAKI na USAWA kwa watanzania wote (wakiwemo masheikh walioko gerezani) na sio kupambana na Mange Kimambi. I stand to be corrected.!!

Malisa GJ
 
Aisee..kama mambo yanasemwa insta...dhidi ya huyu shekhe bac kuna tatizo kubwa sana.....
Hivi ndugu zetu waislamu nyie hayo mambo yaliyowekwa wazi huko inst dhidi ya huyu kiongozi wenu mlikua hamjui au??Manake ni kufuru tupu kwa kiongozi wa dini tena miongoni mwa dini zenye wafuasi wengi kuwa na kashfa nzito kama zile..watu wanatiririka tu kule.....
Bwakata waanzishe uchunguzi juu ya huyu jamaa...anawachafua sana waislamu....kiongozi mkubwa kama yule na yale makashfa bora angejiudhuru akaenda annual retreat hata Muscat huko.....
Zamani niliamini waislamu ni watu ambao hawataki mchezo hasa katika masuala yao ya dini..lkn kwa kashfa hizi za huyu jamaa....jinsi watu wanavyomlalamikia na bila shaka mlikua mnajua .....
 
Na zaidi ukishajiona wewe matendo yako nyuma ya pazia ni machafu bhasi huna haja ya kuanzisha vita na Mange,, ile ig page ya Mange imejaa wadangaji wengi mno wa hapa mjini so manr akikianzisha wao wanamalizs with vivid examples. sheikh anazidi kudhalilika tu kule kwa Mange.ni ngumu kupigana vita ya mtandaoni na Mange
 
Back
Top Bottom