Dar: Soko la Mabegi Karume laungua moto alfajiri ya Aprili 8, 2022

Mbona kuungua kumezidi? Tatizo ni nini? Umeme wa ovyo? Nyaya za umeme za ovyo? Vifaa vya umeme vya ovyo? Yaani nyaya na vifaa vya umeme vilivyo chini ya viwango?
 
Vijana wanjinyima wanapata rizki bado wanachomewa moto mitaji yao, mnataka wawe majambazi?

Wana familia, wana watoto, wana ndugu na jamaa wanawategemea.

Hii nchi ipo siku vijana uvumilivu utawaisha.
Uvumilivu hauwezi kuisha muulize Jenerali Ulimwengu
Tunachoma tujenge mapya mazuri ohooo
 
Soko la mabegi si ndio hapohapo wanauza viatu, na nguo nyingine mbona umeleta habari ya soko lamabegi tu RIRO
 
Kwanza soko hilo lilikuwa na vifaa vya kuzimia moto? Hili jeshi si linatakiwa kufanya ukaguzi huo?
Obviously baada ya matukio ya kwanza ilibidi wafanye angalau kampeni kwa masoko yote kukagua vifaa vya kuzimia moto kama havipo wasupply.

Watoe na elimu ya kuvitumia.

Lakini for years imekua mwendo ni ule ule lakini jeshi bado lipo eti. Kazi imekua ni kuunda kamati ambazo nazo hazitoi suluhu, ni masihara yanaendelea hapa.
 
Dah pigo jingine kwa wajasiriamali wa karume ...yan siku moja baada ya kumbukizi ya mpigania haki KARUME
 
Kwa Nini limeungua moto umetoka wapi na walinzi walikuwa wapi?
 
Kazi na iendelee. Awamu hii ni πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Yule shuhuda wa mchongo, yupo wapi??

Au safari hii watambadilisha??

Pole wahusika wote
 
Mipango miji hovyo sana kuna nyumba zinaweza waka mtaa mzima na kuuzima ikashindikana

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaishi Kwa ujinga zaidi ya Walioishi Karne ya 17!? Masoko yaliungua sana miezi michache iliyopita!! Viongozi hawakuona umuhimu WA kuweka siasa pembeni na kufanyia vitu vya kushirikisha wataalamu!! Hawa OSHA wapo Kwa ajili ya kuuza fire extinguisher mtaani kujipatoa Hela na Sio kuelimisha usalama kazini, kwenye masoko!! My God
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…