Uchaguzi 2020 Dar: Tundu Lissu akamatwa na Polisi, aachiwa bila masharti

Uchaguzi 2020 Dar: Tundu Lissu akamatwa na Polisi, aachiwa bila masharti

Taarifa za hivi punde ni kuwa Vyombo vya Dola jijini Dar vinamshikilia Ndg. Tundu A. Lissu.

Lissu amekamatwa muda mchache uliopita jijini Dar akiwa ameenda Ubalozi wa Ujerumani (amekamatiwa mbele Jengo la Umoja House).

Huu ni mwendelezo wa kukamata viongozi wa CHADEMA na ACT Wazalendo.

======
UPDATE: 1950hrs

Lissu pamoja na wote aliokuwa nao wameachiwa bila masharti yoyote
Naona sasa wakubwa wana hamu na vurugu sana. Nchi imetulia lakini wenyewe wanaendelea kuchokonoa tu.
Tumeambiana tuchape kazi, sasa hizi fuatana fuatana za nini tena.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu mlienda kuandamana?
Uliona wapo polisi wanaogopa maandamano ya Amani kama Polisiccm? Wao tarehe 1 kabla ya mbili wakamkamata mwenyekiti wa chadema kwa kumbambikia kesi wakwawatia hofu waandamanaji
 
Hakuna sababu zingine zaidi ya zile za kisiasa.

CCM ‘imeshinda’ kwa zaidi ya asilimia 80.

Kwa nini ina behave Kama watu walioshindwa na ambao wanatumia mabavu kubakia madarakani?
Sasa hao walio shindwa kwanini wasitulie na wakafanya shughuli nyingine ?
 
Mkuu, jana si ulisema wanamwogopa?
Afande kwema?
20201102_201016.jpg
 
Inawezekana.

Lakini usidharau kabisa mfumo wa usalama wa Tanzania kwa sasa una uwezo mkubwa wa kunasa kila kitu ndani na nje ya mipaka.

Polisi wanafuata maagizo ya intelligence na mashine nzima ya ulinzi na usalama ili Tanzania iwe salama..
Kule Mtwara walishindwa nini kunusa?
 
Back
Top Bottom