Uchaguzi 2020 Dar: Tundu Lissu akamatwa na Polisi, aachiwa bila masharti

Uchaguzi 2020 Dar: Tundu Lissu akamatwa na Polisi, aachiwa bila masharti

Hivi sababu ya kutoakufanikiwa kwa maandamano yenu ni nini?
Maandamano tarehe 2 lakini tarehe 1 Polisiccm wakamkamata mwenyekiti wa chadema na viongozi wengine kwa maana ingine Polisiccm ndiyo wamezuia waandamanaji kwa kutumia vitisho
 
Upinzani ungekuwa unapigania mambo ya msingi haya yote yasingetokea,yule wa CUF anakumbuka shuka wakati kumekucha,eti hawashiriki uchaguzi mwingine wowote kama hakina tume huru.tulisemaga humu toka kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa,kwamba tume huru ni muhimu ikawepo kwanza hata kama tungehairisha huu uchaguzi kwa muda.

Matokeo yake ni kushindwa kama ilivyotokea,walidhani watapata viti vingi vya ubunge kama kipindi cha lowassa.

Sasa kujaribu kuleta sintofahamu,kwa kutishia maandamano imekuwa kama uhaini kwa sasa.kujaribu kutikisa kiberiti cha amani ni hatari.

Mimi naona vyombo vya dola vipo sahihi.na hao mabalozi wakae hapa nchini kwa kutulia.sio wanaletaleta umbea kama mawakala wa shetani.
Mkuu kaa kimia ,unaongea nini,?? Acha kabisa, organ za nchi lazima kupima kabla ya mahamuzi yoyote ,na bila shinikizo lolote,mnashabikia Mambo ambayo yatalighalim taifa? Alafu wakaa wasema we mzalendo?
MH KIONGOZI MH SIRRO ,IGP
Tanzania tuna viongozi wengi ,namanisha rais, viongozi wa upinzani, na wakuu wa vyombo vingi tu,ila Cha kushangaza binfsi wakati napewa maagizo ya kuliombea taifa nilionyeshwa wewe tu kukujumlisha kwenye maombi, na nilifanya hivyo na si mara ya kwanza kusema hili hapa,na mpaka Sasa sijui nini mungu amekuandalia huko mbele mpaka mda huu Sina majibu
Mwisho mkuu
Nakuomba kwa iyo nafasi uliyonayo bila kupesa macho ,hakikisha MH MBOWE ANAACHIWA wenda ikawa aiko ndani ya uwezo wako ila kwa nguvu ya mungu na mkono wake juu yako ni rahis ,NA IMEKUA,naongea na namanisha kiongozi sikujui hunijui ila neema ya mungu niliambiwa ipo juu yako ,mungu akutangulie
 
Na ninachoamini, heri ya hao wanaoshiba utasema ni wabinafsi wanaotetea matumbo lakini am very sure wengine ni malofa wenzetu tu wanaoishi kwa dada zao, na wale wanaokaa kwao basi ni kwenye chumba kimoja choo nje kama sie wengine!

Hawa wanasukumwa sana na Ungosha, and nothing else.

Lakini kama unavyosema, iwe ni wale wenye neema au akina sie, itafika wakati mfumo huu katili utakuwa uchagui, na mfano mdogo ni kwenye hii issue ya Internet... yaani wanaumia waliomo na wasiokuwemo lakini wanaona aibu kusema!!! Yaani wanakufa kifo cha kizungu na tai shingoni!
Mbona mimi siyo ngosha?

Akili kama hizi ndio akikuwa nazo hata Lisu akaishia kupiga kampeni kanda ya ziwa pekee
 
Wakati wamemkamata mbele ya hao mabeberu, yamebaki yanatoa macho tu.
Lissu muoga sana, sasa ndio nini kukimbilia ubalozini?
Waoga ni Polisiccm kwani ndiyo wana Bunduki
 
Ndiyo uko nyumba ya vioo halafu unapiga bomu. Magufuli hachezewi. Na hii ni awamu ya lala salama ni lazima alalishe wasumbufu.

Maandamano hapa hapana kabisa . Kama hujaridhika ni kwenda mahakamani hata ya AFRICA AU DUNIA. Watu maandamano ya Fujo hatujazoeana hayajawahi kutokea tena baada ta yale ya Mwembechai.
Maandamano ya Amani yana fujo zipi?
 
Na kwa sababu walikwisha sema watampiga sindano ya sumu,huu sasa utakuwa ni wakati mwafaka kwao.
Ila wakumbuke,jaribio lolote la kumuua litasababisha mauaji makubwa sana katika nchi hii,na Jiwe atafanyiwa alichofanyiwa rais wa Irak hayati Sadam Husein
Walikuwepo akina Bokasa chiluba Abacha Gadafi Sadam Hussein Elbashiri Iddy Amin dada mabutu wapo wapi?
 
Walikuwepo akina Bokasa chiluba Abacha Gadafi Sadam Hussein Elbashiri Iddy Amin dada mabutu wapo wapi?
Ndiyo kilichobaki sasa kupiga ramli tu mwanzo ulikuwa unasema mnachukua nchi mapema asubuhi. Endelea na ramli zako mkuu!
 
Uanzishe maandamano then ukimbilie ubalozini kweli ni sawa?, Sasa wewe mwananchi andamana then tuone kama utakimbilia kwa balozi wako wa nyumba kumi.
Au unadhani utakimbilia UK Au Germany?

ACHANA NA MAANDAMANO, WATANZANIA TUMESHA AMUA.
Watanzania wa wapi wameamua juu ya CCM? Maana watanzania wenye Akili timamu hawawezi kuipa CCM kura, Yaani wapinzani hawapo huru kwenda popote? mnawachagulia pa kutembelea?
 
Ndiyo kilichobaki sasa kupiga ramli tu mwanzo ulikuwa unasema mnachukua nchi mapema asubuhi. Endelea na ramli zako mkuu!
Na wewe endelea kujinufaisha kupitia blackmail ipo siku utajutia udhalimu wako na wenu
 
Back
Top Bottom