DAR: Vijana watano wamepotea katika mazingira ya kutatanisha

Nadhani mtoa mada yeye katoa tu taarifa kama ilivyo kwenye gazeti
 
Ndugu wamekanusha, hajapasuliwa kokote tumboni
 
Rafiki wa dada yangu mume wake alipotea mwaka jana kama mwezi wa tisa hivi, na yeye pia alikua na wenzake sijui wawili au watatu sikumbuki vizuri ila walikua wanasafiri kuelekea tanga na gari private, Mara ya mwisho mawasiliano yao ilikua wakiwa tegeta baada ya hapo ndio kimyaaa, hadi leo wametafutwa kweli lakini hamna majibu, yule sister keshalia hadi amenyamaza amemuachia Mungu tu.. za kijiweni sasa kule mtaani wanasema eti yule kaka na wenzie ni Wezi wakubwa wa magari kwaiyo wale wamewekwa sehemu undeground sijui wapi hadi chain yote ishikwe..
 
Ukisikia mtu mweusi anamtenga ndugu yake ndio haya sasa. Ujumbe wa Kariakoo na Tanzania kwa ujumla ila mtu kaandika Kikristo.
 
kama ishu zao ni kupika IMEI za simu za wizi basi huo ndio mwisho wao! Polisi huwa ina mtindo wa kuweka records za wahalifu ila kesi ikiwa reccuring huwa wanaamua kuwa eliminate tu kwa namna wanaoijua wao. Ila ni baada ya kuwapa maonyo sana kuwa acheni hio michezo😅
 
Sina elimu.


Basi nisamehe maana ningekudharau Sana Kama unashindwa kutofautisha mambo madogo Kama hayo.

Wapo wanapotea Kwa mambo ya kishirikina,
Wengine Kwa sababu za Mapenzi
Wengine Mali na wauza viungo
Wengine mambo ya Kisiasa.

Hata polisi kabla ya kumtafuta Mtu lazima wajue hadhi yake kijamii ili wabaini sababu ya mtu huyo kupotea ni kisiasa, kijamii au kiuchumi.

Mtu hajihusishi na Siasa atapoteaje Kwa sababu za Kisiasa, hakuna logic hapo.
 
Kama Majambazi ndiyo IMEISHA hiyo ,Polisi wanawapa VYUMA tu.
Hawa nina wasiwasi ni wale wachonga IMEI au wauzaji wa simu za ishu! Ukifuatilia kwa kina utagundua wale waliokamatwa mara kwa mara katika huenda katika maelezo walipoint kuwa dealers wanaowauzia hizo simu ni hawa vijana waliopotezwa. Na kimsingi polisi lazma walishatoa maonyo sana!
 
Mods nqomba muunganishe Iwe faida kwa Swahili audience
 
Kuna kaka wa marehemu alikuwa anasimulia Clouds fm PB.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mkuu umechanganya madesa yule sio kaka yao...yule ni mtangazaj wa clouds anaitwa mbarouk khan. Na yeye alikua anashare tu kisa chake cha kufanana na hvo,jinsi kakake ilivomtokea.
 
Njoo sasa bongo hapa kwa wasiojielewa ukijua kingereza na kuokteza mambo wanakuamini

Mfano mange kimambi na fatuma karume kwa kile kingerza chao wanaonekana watu wa maana na vijana wa ovyo wanawaamini asilimia 100 yaani sijui kwa nn
 
Interesting..
 
Na gari je haikupatikana? Unajua Tanzania tunasema ni kisiwa cha amani ila kuna mambo yanaendelea kimya kimya and no body cares labda mpaka ya kukute ndo unaanza lia lia
 
Haya mambo kwenye ukanda wa Afrika mashariki yanatamaradi sana, kule Kenya napo kuna vijana kadhaa wamepotea na baadae kuonekana eneo lingine pembezoni mwa mto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…