Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kikao cha Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania cha kujadili tuhuma zinazomkabili Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita kimesimama kwa muda baada ya jina la mjumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) kusainiwa wakati hayupo ukumbini.

Kikao hicho kinafanyikia ukumbi wa Karimejee jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 9, 2020 ambacho kabla ya kusimama kilikuwa kikiongozwa na Meya Mwita.

Tukio limesababisha mvutano mkubwa miongoni wa wajumbe wa Chadema na CCM kutaka kushikana mashati wakitakana kupigana.

Mbali na hilo, katika meza kuu hali haikuwa shwari kati ya Naibu Meya, Abdallah Mtinika na Meya Mwita kugombea kipaza sauti wakitaka kuongea ili kutoa ufafanuzi.

Baada ya wajumbe wa Chadema kuingia, Meya wa Ubungo anayetokana na Chadema, Boniface Jacob kushika daftari la mahudhurio na kuhoji uwepo wa jina Kassim Mshamu diwani wa Minazi Mirefu.

"Naomba kutoa taarifa katika hili daftari kuna mjumbe hayupo anaitwa Mshamu ameisaniwa namba 18, lakini mbona hayupo. Mkurugenzi na wewe unasimamia sheria lakini hii sio sawa mmeghushi.”

"Dunia nzima leo inaona mlichokifanya hatuwezi kukubali uhuni mlioufanya leo," amesema Jacob huku akiwaonyesha wajumbe daftari la mahudhurio.

Hatua hiyo ilisababisha mvutano kuzidi kushika kasi hatua iliyosababisha polisi kuingia ndani ya ukumbi ili kutuliza vurugu kati ya wajumbe wa CCM na Chadema.

Polisi baada ya kuingia ndani, wamewatoa ndani ya ukumbi Meya Jacob, Diwani wa Tabata (Chadema), Patrick Asanga kwa sababu hawajasaini daftari la mahudhurio ikiwa ni amri aliyoitoa Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana baada ya kuibuka mvutano wa kutokusaini daftari la mahudhurio.

Meya Jacob amesema hawawezi kusaini daftari ambalo lina makosa ya kughushiwa kwa kuwepo kwa saini ya mjumbe ambaye hayupo.

Lengo la kikao hicho cha madiwani ni kupokea taarifa ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwita baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuchunguza tuhuma ambazo zinamkabili.

Miongoni mwa tuhuma anazokabiliana nazo Mwita ni kutotumia Sh5.8 bilioni za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda). Fedha hizo ni asilimia 51 ya hisa zilizotolewa na kampuni ya Simon Group kama sehemu ya ununuzi wa asilimia 51 ya hisa za Uda.

Tuhuma nyingine ni kutumia vibaya gari ya ofisi ambayo alipata nalo ajali, kushindwa kuongoza kikao cha baraza la madiwani na kusababisha meya wa Ubun-go Boniface Jacob kugombana na meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo na kudaiwa kuwapendelea baadhi ya mameya kuingia kwenye kamati za fedha.

Hata hivyo, Mwita alipofika mbele ya kamati hiyo alishajibu tuhuma hizo akisisitiza hahusiki na jambo hilo bali ni za kutengenezwa ili kuondolewa katika kiti hicho alichokitumikia kwa miaka minne.

--------
Meya.jpg

 
CCM kwa vile hawawezi kukabiliana kwa hoja Bali hila basi dawa yao ni mkono tuu. Boniphace Jacob tembeza mkono ukumbini hadi wajitambue kuwa wao ni mdebwedo tuu.
Kikao cha madiwani lakini nje mnajaza polisi kibao utadhani mpira wa Simba na Yanga?
 
Halafu unamkuta mtu anashangilia hata huu upuuzi,sijui watanzania tumerogwa! Mkuu wa mkoa badala ya kutumia hizo nguvu kutatua kero za wana Dar Es Salaam,yeye yuko busy kuhakikisha Dar iko chini ya CCM! Sijui hata hawajui kuwa na viongozi wengi toka chama tawala ni kumuumiza kichwa Mh Raisi? Maana kazi zote anafanya yeye huku kina RC wa Dar wako busy kushughulika na CHADEMA!
Upuuzi kabisa.
 
Naona Patric Assanga leo alikuwa anaongea sana...Mzee wewe wako ni mkono na tunakuaminia. Hao kenge bila nakoz hawaendi. Emb fanya kama kile kikao ulichokuwa unakamata viwili viwili unatoa discipline.
 
Bashite atabak kuwa bashite tu
Logically Jacob & Co wapo sahihi kutosaini daftari husika kwa kuwa tayari kuna mahudhurio ya KUGUSHI. Sijajua ni akili ipi inatumiwa na wote wanaotaka Mwita 'atemwe' wanafanya makosa ya KIJINGA kiasi hiki! Natumai Makonda ndiye anasimamia huu mchezo, the guy is so pathetic.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom