Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Kuna siku watamuua yule kinara wao yeye ataoza kaburini wewe utabaki unaomboleza. RIP Babu yangu Mwamwindi
Ndio ccm itakuwa imeondoka madarakani?

Siyo kwamba ccm inapendwa hapana! Ni kwamba mbadala wake haupo.

Kiufupi ccm inaendelea kuwepo madarakani sababu ya udhaifu wa wapinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtanyooka tu! Meya ameshapigwa chini hata gari hana na ofc haruhusiwi kuingia. Propaganda zenu huku JF hazifui dafu nendeni mkamchangie pesa za kuishi jijini sasa. Hata kwa Lissu ilikuwa hivi hivi eti hawawezi kumfukuza akapigwa chini na sasa ni kimyaa!!
Unachekelea upumbavu au upumbavu ndo unakuchekesha?
 
Nimefurahishwa sana na njia aliyo onyesha Meya Jacob katika kikao cha Halmashauri ya Jiji la Dar kilicho kuwa kimepangwa ili "kumkomesha" Meya wa Jiji Isaya Mwita baada ya kukataa kuwa na bei ya kuunga mkono juhudi.

Akidi haikutimia kwa wajumbe wa CCM hivyo wakaamuwa kufoji jina la Diwani ambaye hayupo na kusaini.

Jacob akashtukia mchezo na kuchukua attendance register ili kuonyesha ulimwengu hila za CCM katika vikao halali unaofanywa na Mkurugenzi kushirikiana na madiwani na Wabunge wa CCM akiwemo na Mheshimiwa Zungu ambaye ni mwenyekiti wa Bunge asiyepaswa kabisa kushiriki tabia kama hizo.

Walipotaka kumdhibiti kwa kutumia polisi Boniphace alijipanga tayari kutembeza MKONO NA KUNG FU kiasi waka gwaya kumkabili.

Kinachoundwa ni kuhakikisha Meya anakuwa wa CCM kwa gharama yeyote na bila aibu.

Mtindo aliotumia Boniphace ni wakuiga maana CCM hawana aibu hivyo kuna wakati ikibidi kuwapa kichapo ni sawa tu.

Ama kweli 2020 ni #NoHateNoFear
Boni kamchimba biti yule Auxiliary Police kuwa "Mimi nimeshejipanga kwa lolote, nitakuonyesha mfano wa Dunia...Mnatetea wizi hapa...! Njagu alipoona mwanaume hana mzaha hata chembe akaona isiwe kesi....mdogo mdogo akajiondokea [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini ni mambo ya aibu sana. Inatutia doa sana kimataifa.. Huwezi kuamini mambo kama haya yana fanywa na Chama. Kikongwe Afrika.. Yaani nimeangalia ile video nilitamani kulia.. Ccm wana fanya mambo ya aibu.. Hawajui uongozi ni dhamana.. Halafu watatuambia tulinde amani.. Ipi???? Wakati wao ndio wavunjifu wa amani?? Halafu huu upuuzi unafanywa na watendaji wale wale wa TAMISEMI ambao wako ofisi ya rais.. Jamaniii
Hasira za watu bado zipo mioyoni....taratibu zinaanza kutoka na kuwa za wazi. Gap la upendo linaanza kupotea na uadui unashamiri. Tunakoelekea sioni mwanga. Lazima Rais atafute muafaka wa kitaifa. Mbinu za jinsi hii haziwezi kutuunganisha. Mwisho wa siku Tanzania ni moja, vyama vitapita vitakufa lakini Tanzania haitakufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuamini nilipo sikia sauti ya mkurugenzi eti bila ya aibu anaitisha hiyo attendance register eti amfute huyo diwani waliyo mtumia kufoji

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mama Spora Liana ni mama niliyekuwa namheshimu kupita maelezo. Kwanza ni MLOKOLE lakini pia ni mama asiye na kona kona. Leo amenifanya niuone hata UKOKOLE wenyewe hauna maana kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtanyooka tu! Meya ameshapigwa chini hata gari hana na ofc haruhusiwi kuingia. Propaganda zenu huku JF hazifui dafu nendeni mkamchangie pesa za kuishi jijini sasa. Hata kwa Lissu ilikuwa hivi hivi eti hawawezi kumfukuza akapigwa chini na sasa ni kimyaa!!
Unajiita UCD si useme tu unajipendekeza upate UDC? Endelea kujitahidi ili UCD ugeuke kuwa UDC!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hawa wananomshambulia huyu kijana wapo viongozi wa sasa awamu hii na mojawapo hivi sasa ni waziri katika serikali ya jiwe. Inaonekana sifa ya viongozi wengi awamu hii ni ukatili, ufojaji, uropokaji, ulimbukeni na ushamba. Watanzania pia inaonekana tumeridhika kuongozwa na watu aina hiyo la sivyo tungeshachukua hatua za awali za kuwandoa..
anaitwa Jaffo
 
Hii inAniacha hoi sanaaa
Japo its sadness in it!!
Hasahasa huyo jamaa anayekuja na tofari


Sijui km alipona huyo jamaaa
Huyo kamanda Aliwapiga wote hao , unajua wabunge wengi wa ccm wanaumwa Bp na visukari hawana uwezo wa kukimbia hata dk 5 tu !
 
Back
Top Bottom