Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Rais wa wanyonge bado yupo chato? Au yupo ziara kwenye hifadhi za taifa? Nauliza tena vetting ilifanyika kumpata rais wa Tanzania?
Ccm inadhalilisha sana nchi hii,yaani wao vyeo na wizi wa mali za umma ndo priority,nasikitika na kuumia sana kuongozwa na ccm
 
Dawa ya maccm ni kuyatukana... nayachukia maccm nina hasira na maccm ndio maana yana matumbo makubwaaa utadhani sewers
 
ccm ya Magufuli mbende mbende imechoka kabisa wanatumia mbinu za kishambaaaa!!!
 
Ndio ccm itakuwa imeondoka madarakani?

Siyo kwamba ccm inapendwa hapana! Ni kwamba mbadala wake haupo.

Kiufupi ccm inaendelea kuwepo madarakani sababu ya udhaifu wa wapinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkoloni naye alikuwa na mawazo kama yako. Aliamini hakuna mbadala wa yeye kutawala hii nchi. Aliona Nyerere na TANU yake kama waganga njaa tu
 
Haya maagizo ni yapi..Dar ina matatizo mengi sana watu wanaishi kwenye hali duni vikao hivi vinatakiwa kuja na majibu sio kupigana...
 
Wapo wenye uwezo wa kuandika miandiko mitatu mpaka minne tofauti kwa ufasaha kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pitia vitabu vya Forensic Handwriting Analysis; utagundua kuwa mtu yeyote akibadili mwandiko, atajulikana tu. Kuna features ambazo huwa ni vigumu kubadili. Ingawa mimi siyo mtaalamu wa nyanja hiyo, kujisomea kunanisaidia kujua mzchache ya kuanza kuangalia katika kupambanaua miandiko.
 
Nawahukuru Sana hawa Maaskari kwa Kutii kuacha kuninyang'anya Daftari la Mauzulio ambalo CCM waliweka Jina na sahihi ya Mjumbe ambaye yupo Nje ya Nchi. (Wamefoji Mahudhurio)

Nilishafikia Uamuzi wa Kumkamata Askari mmoja Nimng'ang'anie Koo ikibidi nife naye kupinga Uonevu,Dhuluma na Ukandamizaji,Muda Sijui tungekuwa wapi Wote?

Inatia hasira Sana Pale unapoona Kuna Watu wanajiona Wao wanahaki ya kufanya jinai,Kufoji na Uharamia wa kila aina,Mbaya zaidi kwa Kutumia Vyombo vya Dola.

Kilichotolea baada ya Hapa ni Kwamba CCM wakosa 2/3 ya Baraza ambayo ni Kura 17 za kumuondoa Meya madarakani,Wamepiga Kura Zao 16 tuhView attachment 1317315


Ndugu zangu wapendwa, yote haya yana mwisho. Tuombe Mungu atusaidie mwisho wake uwe mzuri na sio mbaya.
Maana wahenga husema "hakuna marefu yasiyo na ncha".
Mungu ibariki Tanzania. Amen
 
Kikao cha Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania cha kujadili tuhuma zinazomkabili Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita kimesimama kwa muda baada ya jina la mjumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) kusainiwa wakati hayupo ukumbini.

Kikao hicho kinafanyikia ukumbi wa Karimejee jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 9, 2020 ambacho kabla ya kusimama kilikuwa kikiongozwa na Meya Mwita.

Tukio limesababisha mvutano mkubwa miongoni wa wajumbe wa Chadema na CCM kutaka kushikana mashati wakitakana kupigana.

Mbali na hilo, katika meza kuu hali haikuwa shwari kati ya Naibu Meya, Abdallah Mtinika na Meya Mwita kugombea kipaza sauti wakitaka kuongea ili kutoa ufafanuzi.

Baada ya wajumbe wa Chadema kuingia, Meya wa Ubungo anayetokana na Chadema, Boniface Jacob kushika daftari la mahudhurio na kuhoji uwepo wa jina Kassim Mshamu diwani wa Minazi Mirefu.

"Naomba kutoa taarifa katika hili daftari kuna mjumbe hayupo anaitwa Mshamu ameisaniwa namba 18, lakini mbona hayupo. Mkurugenzi na wewe unasimamia sheria lakini hii sio sawa mmeghushi.”

"Dunia nzima leo inaona mlichokifanya hatuwezi kukubali uhuni mlioufanya leo," amesema Jacob huku akiwaonyesha wajumbe daftari la mahudhurio.

Hatua hiyo ilisababisha mvutano kuzidi kushika kasi hatua iliyosababisha polisi kuingia ndani ya ukumbi ili kutuliza vurugu kati ya wajumbe wa CCM na Chadema.

Polisi baada ya kuingia ndani, wamewatoa ndani ya ukumbi Meya Jacob, Diwani wa Tabata (Chadema), Patrick Asanga kwa sababu hawajasaini daftari la mahudhurio ikiwa ni amri aliyoitoa Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana baada ya kuibuka mvutano wa kutokusaini daftari la mahudhurio.

Meya Jacob amesema hawawezi kusaini daftari ambalo lina makosa ya kughushiwa kwa kuwepo kwa saini ya mjumbe ambaye hayupo.

Lengo la kikao hicho cha madiwani ni kupokea taarifa ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwita baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuchunguza tuhuma ambazo zinamkabili.

Miongoni mwa tuhuma anazokabiliana nazo Mwita ni kutotumia Sh5.8 bilioni za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda). Fedha hizo ni asilimia 51 ya hisa zilizotolewa na kampuni ya Simon Group kama sehemu ya ununuzi wa asilimia 51 ya hisa za Uda.

Tuhuma nyingine ni kutumia vibaya gari ya ofisi ambayo alipata nalo ajali, kushindwa kuongoza kikao cha baraza la madiwani na kusababisha meya wa Ubun-go Boniface Jacob kugombana na meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo na kudaiwa kuwapendelea baadhi ya mameya kuingia kwenye kamati za fedha.

Hata hivyo, Mwita alipofika mbele ya kamati hiyo alishajibu tuhuma hizo akisisitiza hahusiki na jambo hilo bali ni za kutengenezwa ili kuondolewa katika kiti hicho alichokitumikia kwa miaka minne.


Aliyeunda tume anavyeti feki , pa aligushi jina make jina lake Bashite. Kwenye kikao wamegushi. Hivi unategemea timu kama hiyo iletee watanzania maendeleo?? Ndiyomaana wanagushi hata takwimu za maendeleo. Kila kitu ni mwendo wa kugushi.
 
Magufuli anasema sheria na utaratibu mwingine tuliojiwekea kama taifa unamchelewesha You cant imagine kama huyu mtu yuko hivi na ana elimu ya kiwango cha PhD sasa asinge soma angekuwaje?
Ndugu mbona unatoka nje ya mada na unaanza kuzungumzia watu binafsi?
 
Ndugu mbona unatoka nje ya mada na unaanza kuzungumzia watu binafsi?
Mkuu si tunazungumzia meya wa Dar kutoka kuondolewa kinyume cha taratibu? Sasa huyu niliyemtaja si ndo mwenyekiti wa hao wavunja sheria?
 
AIBUUU SANAAAA HAWA WOTEE WANAKUFAGAAA NA CANCER PALEE OCEAN ROAD MWISHO WA SIKU NA MIFUPAYAOO INANUKA WAKIWA HAII
 
Back
Top Bottom