Dar: Wananchi Mikocheni wagomea Kituo cha Mafuta kujengwa kwenye makazi yao

-Kabla ya kufanya mabadiliko ya matumizi ya ardhi, kunatakiwa kutolewa notisi ya siku kadhaa, kwa yeyote mwenye Pingamizi apeleke kwa Mkurugenzi wa halmashauri,
- Na pia Panatakiwa pafanyike mkutano na Wananchi watoe mawazo yao
 
Nikisoma baadhi ya michango ya wadau napata uzuni kubwa kwa taifa langu Tanzania! Hii mitandao imesaidia sana kubaini uwezo wa fikra za watanzania wa sasa, juzi kulikuwepo mada kuhusu marufuku ya matumizi ya bangi comments nyingi zilionesha ni upuuzi kuzuia matumizi ya kilevi hicho, nikaenda jamiicheck kwenye ufafanuzi wa athari za bangi sikuona comment hata moja au ya kukubaliana na marufuku au kuikataa!

Hii yaja mada ya kituo cha mafuta kujengwa kwenye barabara ya huduma za dharura kwenye makazi ya watu (access road) bado kuna wanaoona marufuku ya ujenzi huo ni upuuzi, kwamba hawajui umuhimu wa access roads, kwamba hawajui athari za kituo cha mafuta katikati ya makaazi ya watu (japo aliyechomoa battery kule msamvu miaka fulani) alama ya athari zake ipo mpaka leo lakini hapa kuna watu hawawazi kwamba hata kituoni hapo battery yaweza chomolewa pia. Lakini hawajui kama huwa kuna mipango miji yenye master plan inayoonesha kila ardhi na matumizi yake, na kwamba mkuu wa wilaya anaposema atachunguza vibali alivyokutwa navyo bwana mwekezaji kama vilipatikana kiharari yupo sahihi!

Hutimisho, hatuwezi kuendeleza uhalifu eti kisa uhalifu huo unatendeka kwa wengine wawe waburuza ndala au vigogo.
 
Kama hujui abc za mipango miji lazima uongee pumba kama hii ujinga ni mzigo
 
Hata mkuu wa wilaya hajui taratibu za mipango miji
Tanzania ni nchi iliyopo gizani
 
"Mkazi mwingine wa eneo hilo, Profesa Anna Tibaijuka amesema kituo hicho cha mafuta kinajengwa kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria"
 
Kuna gas station moja ya Puma ipo Survey pale, huwa naitazama nashindwa kuelewa ilikuaje ikajengwa pale...

Kuna gas station nyingine ipo barabara ya Msewe (jina lake silijui), ila ipo katikati ya makazi ya watu, sijui walipataje vibali wale...
 
Wananchi wamefungua macho sasa. Sisi mtaani kwetu tumezubaa hadi kituo kimefunguliwa kiwanja cha makazi ya watu maana hatukutangaziwa mabadiliko ya matumizi.
 
Kwamba unavyoona kwa akili yako mkuu wa wilaya yuko sahii
Yuko sahihi ndio kwa sababu amejipa muda wa kuchunguza vibali alivyo navyo mwekezaji ili kubaini kama ni harari ndipo arudi kwa wakaazi wa eneo kuwapa majibu ya hatua zitakazofuata.
Huoni kama kafuata utaratibu sahihi?
 
Vituo vyote viko karibu na makazi akiona vipi arudi UN Habitat aje mpango kazi vituo vikae hewani sasa....anataka viwe karibu na makazi ya wadudu ? Kote kote kuna makazi na vituo vipo niambie kituo kilicho mbali na makazi watu ? Atuondelee umaarufu na kick zake
 
Bangi na Sigara ipi ina madhara makubwa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…