Dar: Wananchi Mikocheni wagomea Kituo cha Mafuta kujengwa kwenye makazi yao

Dar: Wananchi Mikocheni wagomea Kituo cha Mafuta kujengwa kwenye makazi yao

Vituo vyote viko karibu na makazi akiona vipi arudi UN Habitat aje mpango kazi vituo vikae hewani sasa....anataka viwe karibu na makazi ya wadudu ? Kote kote kuna makazi na vituo vipo niambie kituo kilicho mbali na makazi watu ? Atuondelee umaarufu na kick zake
Kituo cha mafuta kinatakiwa kikae umbali gani na makazi ya watu, shule au hospitali?
 
Yuko sahihi ndio kwa sababu amejipa muda wa kuchunguza vibali alivyo navyo mwekezaji ili kubaini kama ni harari ndipo arudi kwa wakaazi wa eneo kuwapa majibu ya hatua zitakazofuata.
Huoni kama kafuata utaratibu sahihi?
Swala sio utaratibu hao wananchi hawajashirikishwa kabisa kama sheria inavyosema tayari huo mchakato mzima ni haramu
 
Wananchi wakazi wa Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi, Kata ya Mikocheni wilayani Kinondoni Dar es Salaam wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao.

Kituo hicho kinajengwa katika Barabara ya Senga, Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi Kata ya Mikocheni.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa huo, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema sheria ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi haikufuatwa kabla ya ujenzi huo.

Mwananchi huyo ambaye amejitambulisha kuwa yeye ni mtaafu serikalini, alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi huo, sheria inamtaka mtu anayetaka kubadilisha matumizi ya ardhi kushirikisha wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka matangazo eneo la wazi kwa muda wa siku 21 ili kama kuna pingamizi litolewe.
View attachment 2814581
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (mwenye suti) kushoto akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mikocheni kuhusu madai ya ujenzi wa kituo cha mafuta katika makazi ya watu.

“Haya mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika eneo hili haikutushirikisha, matangazo hayakuwekwa. Tumekuja kushtuka ujenzi umeanza.”amesema mwananchi huyo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Profesa Anna Tibaijuka amesema kituo hicho cha mafuta kinajengwa kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

“Kwanza barabara hii si barabara kuu, hii ni access road (barabara ndogo ya mtaani), huyu anajenga kituo cha mafuta, yatakuja magari maroli makubwa hapa hakuna hata nafasi, barabara hii ni finyu sana, na si eneo zuri kwa usalama na afya za wananchi ” alisema Profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka ambaye amepata kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema kuwa suala hilo tayari wamelifikisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye analishughulikia.

“Tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya ameanza kulishughulikia kwa kufika eneo kinapojengwa kituo hiki cha mafuta, tunaamini suala hili litapata ufumbuzi.”aliongeza Profesa Tibaijuka.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amekiri kupokea malalamiko hayo na wananchi wa Mikocheni.

“Kweli nilipokea malalamiko ya wananchi hao, jana nilikwenda kujionea mazingira ya kituo hicho kinachojengwa, nilichokigundua kampuni inayojenga kituo hicho inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha Baraza la Mazingira (NEMC).
View attachment 2814583
“Ni kweli nilipokea malalamiko ya kituo cha mafuta kujengwa katika makazi ya watu, jana nilikwenda (Novemba 14,2023) kujionea mwenyewe.

“Nilichokigundua ni kwamba hiyo kampuni inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha NEMC (Baraza la Mazingira), hatua inayofuata sasa ni kuangalia kama zile hatua za utoaji wa vibali hivyo ulifuatwa au kuna kilichokosewa. Baadaye nitakwenda kuwaeleeza wananchi tulikofikia”alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni.

Mmoja wa makandarasi wanaosimamia ujenzi wa Kituo hicho (jina tunalo), alipopigiwa simu kuzungumzia suala hilo, aliahidi kupiga simu baadaye. “Nitakupigia, subiri”ulisomeka ujumbe wa simu kutoka kwa mkandarasi huyo.

Chanzo: MATUKIODAIMA
Aliyekosea kutoa vibali ajiandae kumlipa fidia kubwa sana, utasikia tunalipishwa bilioni 500 kwa hicho kituo
 
Huo ndiyo unaitwa ushirikishwaji wananchi katika mipango miji. Inatakiwa mradi au jengo tofauti na yaliyopo ktk eneo husika kukubaliwa na wakaazi.

Siyo kwa kuwa umenunua eneo basi unaweza kufanya lolote bila kujali wakaazi wa eneo hilo wanalikubali au kukataa madhumini ya matumizi ya eneo lako.
Hao wakazi wakati wanajenga makazi yao walimshirikisha nani?
 
Kituo kitajengwa tu, kwa ccm hii ya samia, Mungu wao ni pesa na Rushwa, hapo mihamara itatembea kuanzia, serikali za mtaa, mpaka wizarani, na kituo kitajengwa.
 
Licha ya kuwa ni idea nzuri ila sioni point zao,
At the end hicho kituo kitajengwa tu,
Huwezi sema kisa ni Access road hivyo haistahili uwepo wa kituo cha mafuta, + kuhusu eneo kwani hiyo sheli itakuwa inakaa na magari all the time?

Mimi binafsi sioni kama wana point,
wewe mjinga utajengaje Petro station kwenye makazi ya watu? nchi inaharibiwa sababu pia ya wapumhavu type yako.Mko wengi sana nchi hii mkoa karibia million 57 mwenye akili za aina hii
 
09 December 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Wakaazi waendelea kuchachamaa kituo cha mafuta

PROF. TIBAIJUKA AIBUKA, MZEE RUPIA / HAPA KUNA MCHONGO / HATUNA PAKWENDA / RC CHALAMILA TUSAIDIE / SHELI HII IONDOKE


View: https://m.youtube.com/watch?v=67q1DVoGjcI
Albert Chalamila - Nyaraka zinaweza kuwa za kweli, lakini hazikufuata taratibu na sheria za mipango ya miji hivyo nitachunguza hivyo naomba mnipe muda, mimi hapa RC mkuu wa mkoa ninashitakiwa kesi kibao hivyo tunahitaji umakini jinsi tunavyoendea mambo kama haya ...
 
Back
Top Bottom