Kuna ka "ujinga" kanapita mitandaoni eti kuna watu walijaribu kumuhonga waziri Jerry Silaa. Takukuru wapo, na namba zao anazo, na huwa wanaweka mitego kunasa watoa rushwa.
Waziri ni kiongozi wa ngazi ya kitaifa, ana namba ya boss wa takukuru, kwa nini hakuweka mtego?
Walijadiliana halafu hazikutosha akaona awahi kuwalipua? Aliwaomba hizo hela wakasema hawana akaona awawahi?
Waziri analalamika, wanajimbo wake wafanyeje? Waziri yuko karibu na kila taasisi?
Huyu ataongoza vita ya rushwa wizara ya ardhi wakati hajui sehemu ya kuripoti rushwa?
Useless,aliomba akanyimwa, mawaziri vijana, acheni tamaa, Samia,kazi kwako.
Naona kaitisha umiliki wa ardhi wa vituo vya mafuta nchi nzima, maokoto yake sio mchezo, kamishna wa ardhi atakayepeleka maokoto mengi ndiye atadumu. Anadhani watampa hela za bure (rushwa) ili asivunje vituo vyao
Ajue tu, kodi ya mafuta ndio injini ya bajeti, na mafuta yameangusha wanasiasa wa mashariki ya kati, kabla hajaangusha serikali ya samia, ataanguka yeye. Kama kajipanganga kubomoa vituo vya mafuta nchi nzima, nchi nzima itambomoa yeye.