Hivi kuna mtu angefungua kituo cha mafuta kama hakuna magari ya kujazia.
Gharama tu za mishahara, uwezekaji, tozo za serikali ambazo uuze usiuze lazima ulipe, mkopo wa bank na admin costs nyingine ambazo wauza mafuta wanaweza tutajia kwa kina.
Mpaka watu watake kuwekeza huko kuna demand ya kutosha.
Takwimu zinaonyesha kuanzia 2007 mpaka 2015 kwa mwaka zaidi ya magari laki 3 yanasajiliwa kila mwaka.
Hivi unadhani bila ya nyongeza ya vituo si ingekuwa foleni kwenye kujaza, inconvenience ya kufuata vituo mbali na unapoishi, si ajabu wengi wenu wenye magari mngekuwa mnatembea na madumu spare kwa sababu ya umbali wa vituo.
Sasa kuanzia 2015 mpaka 2023 si ajabu kila mwaka nchi imepita registration ya magari laki nne kwa mwaka.
Watanzania huwa wanalalamikia vitu vyenye faida kwao, mpaka watu wanapofanya maamuzi ya kijinga huko serikalini wakishaanza kuona madhara yake wanaanza kulalamika.
Ni ujinga kupambana na wawekezaji kwa sababu za ovyo, kuna safety measures ya hivyo vituo kunapo madhara ya mlipuko; hawapewi tu vibali kiholela na EWURA.