Dar: Watu 7 wapofuka Macho kwa kujitibu Ugonjwa wa 'Red Eyes' kienyeji

Wizara ya Afya imesema idadi ya watu waliopata upofu jijini Dar es Salaam kutokana na kutibu ugonjwa wa macho mekundu kwa njia za kienyeji wamefikia saba kutoka wanne.

Februaru 8, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Ruggajo alisema watu wanne waliougua ugonjwa huo wamepata upofu kwa kujitibu kienyeji.

Ugonjwa huo wa maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi la jicho unaoitwa Conjunctivitis, maarufu Red eyes umeshasambaa katika mikoa yote nchini.

Februari 7, mwaka huu, mratibu wa huduma za afya msingi na matibabu ya macho Zanzibar, Dk Rajab Muhammed Hilali alitoa takwimu za watu saba kupata upofu baada ya matumizi ya dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo.

Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.
Ila wenetu DSM mna maisha magumu sana.

Yaani mnashindwa hata kwenda vituo vya afya mkapata ushauri mzuri.
 
Wizara ya Afya imesema idadi ya watu waliopata upofu jijini Dar es Salaam kutokana na kutibu ugonjwa wa macho mekundu kwa njia za kienyeji wamefikia saba kutoka wanne.

Februaru 8, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Ruggajo alisema watu wanne waliougua ugonjwa huo wamepata upofu kwa kujitibu kienyeji.

Ugonjwa huo wa maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi la jicho unaoitwa Conjunctivitis, maarufu Red eyes umeshasambaa katika mikoa yote nchini.

Februari 7, mwaka huu, mratibu wa huduma za afya msingi na matibabu ya macho Zanzibar, Dk Rajab Muhammed Hilali alitoa takwimu za watu saba kupata upofu baada ya matumizi ya dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo.

Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.
da!!! wantengeneza sabasaba,zanzibar saba wamepofuka,dar napo saba!!!
 
Mkuu usinikumbushe hayo mambo, awamu ya 5 ukiitafakari ni kwamba hii nchi wote tuligeuka vichaa.
Mengi yalifanyika hadi huwa nahofia tutawajibu nini watoto wetu, tulikuwa wapi wakati yote hayo yanatokea?
Kwahiyo machanjo ya corona ndio DAWA?
 
Hawa wahuni tu.
Hawa walishadidia kupiga "nyungu" na miti isiyoeleweka wakati wa Corona.
Watupe takwimu watu wangapi walikufa kwa kupiga nyungu mkorogo!
Mshamba wewe, hujui nyungu ni tiba inayatambulika badala yake unataka kubugia machanjo ya ulaya.

Piga nyungu mwili unakuwa safi.

Samia mwenyewe anapiga nyungu kisiri siri anawazuga nyie manyumbu mkadungwe machanjo yenye sumu.

Yeye akaaaa... chanjooo!!! Mweeeh 😂😂😂
 
Hadi maduka ya uchochoroni zipo dawa za matone ya macho, au watu wanaona mzuka wakiambiwa tia mafuta ya taa au mkojo wa punda wanajua hiyo ni komesha ya ugonjwa, kumbe wanaishia kukomesha macho yao wenyewe....
Mshamba wewe, mkojo wa punda ni dawa tena dawa yenye nguvu kweli kweli.

Zamani tulipokuwa wadogo tukipata mapele na matetekuwanga tunaogeshwa kwa mkojo wa punda na tunapona.

Vidonda na mapele yote yanaisha. Ngozi inabaki safiiiiii, laiini na nyororo kama sakafu.

Nyie wazee wa machanjo kila kitu mnatega tako mnadungwa sindano.

Hata ukijikwaruza kidogo unakimbilia kudungwa machanjo ya makalio.

Bure kabisa, machanjo hovyo kabisa
 
Zaman kijjn huko, ukiumwa macho unaambiwa uende kwa mama anayenyonyesha akukamulie maziwa kdg machoni na unapona ,,,,,

Rural life
 
Siyo suala la fedha tu, ni suala la mass ignorance. Unakumbuka Magufuli na korona? Magufuli alifanikiwa kuteka nchi yote kuwa kujifukiza ndiyo dawa ya korona?
Unataka kuniambia hakuna elimu yoyote iliyotolewa juu ya ugonjwa huu?! Mass ignorance?!
 
Hata kama ilitolewa haiwezi kuondoa mass ignorance. Mass ignorance inaenda beyond... mass ignorance inazuia hata elimu za kawaida za darasani zisifanye kazi.
 
Mshamba wewe, mkojo wa punda ni dawa tena dawa yenye nguvu kweli kweli.

Zamani tulipokuwa wadogo tukipata mapele na matetekuwanga tunaogeshwa kwa mkojo wa punda na tunapona.

Vidonda na mapele yote yanaisha. Ngozi inabaki safiiiiii, laiini na nyororo kama sakafu.

Nyie wazee wa machanjo kila kitu mnatega tako mnadungwa sindano.

Hata ukijikwaruza kidogo unakimbilia kudungwa machanjo ya makalio.

Bure kabisa, machanjo hovyo kabisa
Huna akili hata kidogo, kwa hiyo tufungashe mikojo ya punda kama dawa ya kutibu wagonjwa huko mahospitalini?
 
Back
Top Bottom