Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 40,828
- 99,523
Huyu jamaa ni ndugu yangu wa karibu kabisa. Yaani ni mjukuu wa shemeji yake na binamu wa mamaangu wa kambo.
Ni siku ya tatu sasa tangu nifike hapa mjini, baada ya kuuza ng'ombe nikaona sio mbaya nikaosha kidogo macho na ning'arishe ngozi kwa maji ya mwambao.
Sasa nilifikia kwa huyu ndugu yangu wa karibu kabisa. Kwakweli walinikaribisha uzuri na sote tulifurahi na kukumbushana habari za majirani wa kule kijijini, siku hiyo walinitandikia jikoni na nikalala bila tatizo hadi ikawa asubuhi.
Nilipo amka nikakuta sebleni wameweka chai mezani na kamkate kamoja, mie nikakakata vipande viwili nikaloweka kwenye chai nika kakula kakaisha. Kwanza chai yenyewe niliona niweke kwenye bakuli la kunawia na ikaishia humo, maana tuvikombe niliona twa watoto.
Kisha nikaondoka nikaenda kwenye genge la jirani nikanunua viazi ili nikazie maana nilikua sijashiba.
Mchana nilipo rudi, nikakuta ugali umepikwa kidogo kama kilo mbili tu, mie nikaula ukaisha na ile mboga nikamaliza yote hadi mchuzi nikaunywa.
Sasa nilipo rudi jioni nikawekewa kikao na mke wa ndugu yangu kwamba nina tabia mbaya, nami nikamuuliza "tabia gani"? Akajibu kwamba sifai kukaa kwake, basi nikasema kwamba hakuna tatizo. Nikaenda kulala na kwakua ndugu yangu alichelewa kurudi, yule mama akaniambia kesho ananiaga na niondoke.
Mie huyooo nikaingia jikoni, nikawapanga kuku wao pale nami nikaweka tandiko nikalala. Kesho yake palipokucha nikawahi kuamka asubuhi nikijua leo ninaagwa, basi nikakamata jogoo (kama desturi yetu kule kijijini tunapo muaga mgeni) nikamchinja na nikamuweka kwenye beseni nikisubiri wenyeji wangu waamke wanipikie kuku ili nile niondoke.
Lahaula! Kilicho tokea baada ya wenyeji wangu kuamka ni siri yangu wakuu. Ila kumbe watu wa Daslam mnaroho mbaya sana wallah, na hamtokaa mnione tena ndio mtajuta..🤨😑