Dar watu wana roho mbaya sana, nimeamua nikalale stendi kesho nirudi zangu mkoani

Na jinsi ulivyokuwa unapiga mswaki na taulo barabarini mbele nyumba, halafu bado hawajaua ulichukua kipande cha sabuni ya kuoshea vyombo uani ukaogea na kuirudisha kimyakimya.....
Kwa kweli ilibidi tu wakutoe mkuku.....
 
Sikua na taulo mkuu, nilikuna na kaniki "shuka jeusi" na mswaki wa gome "mti"
Na bahati nzuri tangu nifike sikuoga, kwahiyo sabuni yao sikuitumia kabisa...🤗
 
🤣🤣🤣
Kwa hiyo na joto lote la Dar , ulikuwa unapiga passport size....
Basi uliwachosha na vituko vingi mpaka wakakuchoka....
 
Punguzeni roho mbaya mkuu, kwani nisipo oga mwili ni wenu..??
Ndiomaana kwa kuwakomesha nimeondoka nikalale stendi, kesho nirudi zangu kijijini...😕
 
🤣🤣🤣 wakomeshe kabisa

🤣🤣🤣🤣
Ndio maana kesho yake nilipopita jikoni nikaona wametenga kafugo kadogo, niliamua kubadilisha nikaongeza na maji.....
Sasa kilicho nikwaza eti binti wao wa kazi akanishangaa kama nimetenga maji yakuoga na joto lote la Dar, nikamjibu "pika ugali huo biti"
 
Back
Top Bottom