BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,122
- 4,060
...Kwanza Sahihisha Hapo..Subri waje watu wa daslam
Huyo Jamaa Sio Ndugu in Yako wa Karibu!
Undugu unapata Kizunguzungu Kuelezea Ukoje??[emoji848]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...Kwanza Sahihisha Hapo..Subri waje watu wa daslam
...Unafikaga Kwa Watu huendi Hata na Unga ama Mfuko TU wa Sukari?Sikua na taulo mkuu, nilikuna na kaniki "shuka jeusi" na mswaki wa gome "mti"
Na bahati nzuri tangu nifike sikuoga, kwahiyo sabuni yao sikuitumia kabisa...[emoji847]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Ulitaka ugari mkubwa,je ulibeba debe la unga ??.Mgeni kujichinjia kuku bila idhini ya mwenyeji ni fujo sio ustaarabu,hukufanya vizuri.Kwa hiyo na sisi tukija kwako tufanye hivyo hivyo???.Kwani hawakujua kama mimi ni mgeni hadi nijichinjie kuku..??
Alafu ugali walikua wanapika mdogo sana mkuu, na kwao sikanyagi tena hadi wakome....[emoji53]
Haieleweki hii aisee"Yaani ni mjukuu wa shemeji yake na binamu wa mamaangu wa kambo."
Hahahahaha.... umenichekesha sana mkuu!!Huyu jamaa ni ndugu yangu wa karibu kabisa. Yaani ni mjukuu wa shemeji yake na binamu wa mamaangu wa kambo.
Ni siku ya tatu sasa tangu nifike hapa mjini, baada ya kuuza ng'ombe nikaona sio mbaya nikaosha kidogo macho na ning'arishe ngozi kwa maji ya mwambao.
Sasa nilifikia kwa huyu ndugu yangu wa karibu kabisa. Kwakweli walinikaribisha uzuri na sote tulifurahi na kukumbushana habari za majirani wa kule kijijini, siku hiyo walinitandikia jikoni na nikalala bila tatizo hadi ikawa asubuhi.
Nilipo amka nikakuta sebleni wameweka chai mezani na kamkate kamoja, mie nikakakata vipande viwili nikaloweka kwenye chai nika kakula kakaisha. Kwanza chai yenyewe niliona niweke kwenye bakuli la kunawia na ikaishia humo, maana tuvikombe niliona twa watoto.
Kisha nikaondoka nikaenda kwenye genge la jirani nikanunua viazi ili nikazie maana nilikua sijashiba.
Mchana nilipo rudi, nikakuta ugali umepikwa kidogo kama kilo mbili tu, mie nikaula ukaisha na ile mboga nikamaliza yote hadi mchuzi nikaunywa.
Sasa nilipo rudi jioni nikawekewa kikao na mke wa ndugu yangu kwamba nina tabia mbaya, nami nikamuuliza "tabia gani"? Akajibu kwamba sifai kukaa kwake, basi nikasema kwamba hakuna tatizo. Nikaenda kulala na kwakua ndugu yangu alichelewa kurudi, yule mama akaniambia kesho ananiaga na niondoke.
Mie huyooo nikaingia jikoni, nikawapanga kuku wao pale nami nikaweka tandiko nikalala. Kesho yake palipokucha nikawahi kuamka asubuhi nikijua leo ninaagwa, basi nikakamata jogoo (kama desturi yetu kule kijijini tunapo muaga mgeni) nikamchinja na nikamuweka kwenye beseni nikisubiri wenyeji wangu waamke wanipikie kuku ili nile niondoke.
Lahaula! Kilicho tokea baada ya wenyeji wangu kuamka ni siri yangu wakuu. Ila kumbe watu wa Daslam mnaroho mbaya sana wallah, na hamtokaa mnione tena ndio mtajuta..🤨😑
Mtu mwenye stor ya kueleweka hawez chinja kuku isiyo yake kwenye mji usio wake bila taarifa wala ruhusa af akasubiria achemshiwe supuKwani haujaelewa wapi mkuu...??🤔
😄😄😁mkongwe kilikujuta niniHuyu jamaa ni ndugu yangu wa karibu kabisa. Yaani ni mjukuu wa shemeji yake na binamu wa mamaangu wa kambo.
Ni siku ya tatu sasa tangu nifike hapa mjini, baada ya kuuza ng'ombe nikaona sio mbaya nikaosha kidogo macho na ning'arishe ngozi kwa maji ya mwambao.
Sasa nilifikia kwa huyu ndugu yangu wa karibu kabisa. Kwakweli walinikaribisha uzuri na sote tulifurahi na kukumbushana habari za majirani wa kule kijijini, siku hiyo walinitandikia jikoni na nikalala bila tatizo hadi ikawa asubuhi.
Nilipo amka nikakuta sebleni wameweka chai mezani na kamkate kamoja, mie nikakakata vipande viwili nikaloweka kwenye chai nika kakula kakaisha. Kwanza chai yenyewe niliona niweke kwenye bakuli la kunawia na ikaishia humo, maana tuvikombe niliona twa watoto.
Kisha nikaondoka nikaenda kwenye genge la jirani nikanunua viazi ili nikazie maana nilikua sijashiba.
Mchana nilipo rudi, nikakuta ugali umepikwa kidogo kama kilo mbili tu, mie nikaula ukaisha na ile mboga nikamaliza yote hadi mchuzi nikaunywa.
Sasa nilipo rudi jioni nikawekewa kikao na mke wa ndugu yangu kwamba nina tabia mbaya, nami nikamuuliza "tabia gani"? Akajibu kwamba sifai kukaa kwake, basi nikasema kwamba hakuna tatizo. Nikaenda kulala na kwakua ndugu yangu alichelewa kurudi, yule mama akaniambia kesho ananiaga na niondoke.
Mie huyooo nikaingia jikoni, nikawapanga kuku wao pale nami nikaweka tandiko nikalala. Kesho yake palipokucha nikawahi kuamka asubuhi nikijua leo ninaagwa, basi nikakamata jogoo (kama desturi yetu kule kijijini tunapo muaga mgeni) nikamchinja na nikamuweka kwenye beseni nikisubiri wenyeji wangu waamke wanipikie kuku ili nile niondoke.
Lahaula! Kilicho tokea baada ya wenyeji wangu kuamka ni siri yangu wakuu. Ila kumbe watu wa Daslam mnaroho mbaya sana wallah, na hamtokaa mnione tena ndio mtajuta..🤨😑
Unafaa Sana kwa comedy/vichekeshoSubri waje watu wa daslam