Baada ya Ibada ya kuuombea na kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kufanyika katika kanisa la St Peters Jiji Dar es Salaam sasa ni muda wa uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam. Wananchi wamekusanyika kwa wingi kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania
WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA RAIS MAGUFULI
Wakazi wa Dar wamejitokeza barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
Wameonekana kutandika Khanga barabarani, wengine walibeba mashada na mabango yenye ujumbe
----
Wakazi wa Dar wamejitokeza barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Wakazi wa Dar walionekana kutandika Khanga barabarani ili magari yaliyobeba mwili wa Hayati Magufuli yapite juu yake kuonesha heshima.
Wananchi wengine walikuwa wamebeba mashada ambayo walikuwa wakiyapunga mwili wa Marehemu ukiwa Unapita kuelekea Uwanja wa Uhuru.
View attachment 1729992View attachment 1729993View attachment 1729994View attachment 1729995