Kutokana na kulipuliwa Kwa daraja, Putin amesusa kusambaza ngano
Mytake:Kama Putin anatumia daraja kupitisha silaha ili kushambulia Ukraine kwanini lisilengwe?
+
++Ikulu ya Urusi Kremlin imesema hii leo kuwa inajiondoa kwenye makubaliano ya usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi, saa chache baada ya ndege zisizo na rubani kushambulia daraja la Kerch ambalo ndilo pekee linaloiunganisha Urusi na Rasi ya Crimea. Makubaliano hayo muhimu ambayo kwa mwaka jana pekee yalisaidia kusafirishwa kwa shehena ya tani milioni 32 za nafaka, yalifikiwa ili kupunguza hofu ya uhaba wa chakula duniani hasa katika nchi zilizo hatarini zaidi. Ni zipi athari za uamuzi huu hususan kwa mataifa ya Afrika?
+++Umoja wa Ulaya hii leo umekutana na viongozi wa Amerika ya Kusini na visiwa vya Karibiki, huku wakiwa na matumaini ya kurejesha upya uhusiano ulioingia doa kufuatia mgawanyiko mkubwa juu ya biashara na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Kwenye mazungumzo yao, Umoja wa Ulaya umeashiria kufanya uwekezaji mkubwa kwenye mataifa ya kanda hizo kwenye miradi mbalimbali.
Source: DW Kiswahili