Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara

Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
10,508
Reaction score
23,368
Daraja la Mkange katika Kijiji cha Magubike wilayani Kilosa mkoani Morogoro limebomoka kwa mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mawasiliano kati ya Dodoma na Morogoro kukatika.

======

Daraja la Kiyegeya lililopo wilayani Gairo kati ya Magubike na Kiegeya Barabara ya Morogoro-Dodoma limekatika, hivyo hakuna mawasiliano. Wanaotoka au kuelekea Dodoma wanashauriwa kuahirisha safari au kupitia Iringa.

1583162219671.png


FE5B62B0-D869-4882-8E73-3EAE4E63F656.jpeg

UPDATE
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kumalizika leo Machi 03, 2020 usiku na ifikapo majira ya saa 3:30 usiku magari yataanza kupita

 
Tushukuru kwa kila jambo.Tunashukuru Mvua kwa kutuvunjia daraja,wazee wa kilosa tumieni fursa kufanya biashara ya mabasi kwa wale waliokwama wauzieni chakula.Nimemiss kilosa aisee.

Ahsante JPM mvua ya baraka imenyesha kwa ajili ya utukufu wa awamu ya 5.Ahsante baba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#BREAKINGNEWS: Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw. Loatha Ole Sanare ametangaza kufungwa kwa barabara ya Dodoma-Morogoro kutokana na kukatika kwa daraja la Kiyegeya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom