haya mkuu,inaonyesha unataka kusema hizo addiction zingine ziko less destructive na hivyo mtu kuchagua kutumia madawa ni maamuzi ya kijinga sababu madawa yako more destructive..
.sio kweli kuwa hizo addiction zingine ziko less destructive ,mfano Water inaweza kukuletea majanga kama utakunywa maji mengi in short time(water intoxication), food nayo kwa wingi nayo inaweza kuleta heart attack..etc
SAD,addiction is a process,one become addict not overnight but for a period/time,ndio maana hatujui mtu kwa mfano kama mwanamuziki Darasa anatumia madawa mpaka tumuone aki behave strangely in which case its too late sababu inakua atakua tayari ameshayatumia kwa muda….
halafu usiseme 'kapenda'...you have never been in his shoes and understand his daily struggle..
hizo unazoziita sababu zisizo na mashiko,ndizo hizo hizo zinazokuwa overlooked na mtu hapati msaada….mie nimefikiria kuwa msaada wa kitabibu inawezekana ni vigumu,ila tunaweza kwa pamoja kuishauri familia yake..
binafsi,sio mtaalam wa mambo haya,ila nafikiri,KUONDOA vitu vyote ambavyo vina act as reinforcers for him to seek self stimulation itakuwa first step...
Mdada uko na akili sana.
I guess utakua mtu wa health profession, au mwanasaikolojia/mshauri nasaha au taaluma inayofanana na hizo. If not,then hats off.
Nikija kwenye mada kuu, unajua kwenye masuala mazima ya addiction, sehemu kubwa ya tatizo ni hiki unachokiona hapa!! Lawama, kuona waliodumbukia katika addiction ni wakosaji sana na wapumbavu sana, kuwasema sana, na kadhalika. Hapo bado hujakutana na mifumo ya kiserikali na/au kipolisi ambayo inaweka mbele zaidi kuwatia jela/korokoroni wahanga wa addiction kuliko kuwapa msaada wa kitabibu na/au kisaikolojia.
Kuna sababu nyingi kweli za kupelekea addiction (za kitabibu, kisaikolojia, kijamii).
Watu hawaelewi kuwa hata ugonjwa wa akili pia unaweza kusababisha mtu akadumbukia katika uvutaji unga/bangi na kupelekea hadi katika addiction(ndio, drug abuse and addiction inaweza ikawa ni dalili ya ugonjwa wa akili!!).
Tukiachana na hayo, kama walivyoshuhudia wengine kwenye huu uzi kuwa Darasa alianza hizo tabia tangu kitambo kabla hajawa maarufu. Je, tunajua mazingira aliyokulia? Washikaji zake aliokua nao wakati anastruggle kutoka, je wangapi sio wahanga wa unga? Hao ndugu zake ambao inaripotiwa "wamemfungia" (kama ni kweli,na i hope sio kweli, bali wamempeleka sober house), je,angekua sio maarufu wangemfungia? Wamemfungia kumsaidia au kukwepa wao wasiaibike??
Watu hata hawajiulizi kwa watu kama hawa wasanii, je wana msaada gani wa kisaikolojia na/au kijamii katika kuendesha maisha yao pale ambapo wanapata umaarufu na pesa mara nyingine kwa ghafla na kwa mkupuo...(au inapotokea kinyume chake).
Hata hao wanaopiga kelele kwa hii thread, si ajabu ukiwapitisha kwenye mapito yale yale aliyopitia Darasa, asilimia 75 unaweza kukuta wanaishia kwenye mkumbo huo huo.
Hivi BASATA wamewahi hata kusugua vichwa vyao na kujiuliza wafanye nini kusaidia kupunguza wimbi hili la wasanii kudumbukia kwenye kubwia unga?
Alamsiki.
Rebeca 83
Sent using
Jamii Forums mobile app