Darasa la saba waliopata maksi 60 nao kubebwa kwenda sekondari - Agizo la Kikwete

Darasa la saba waliopata maksi 60 nao kubebwa kwenda sekondari - Agizo la Kikwete

Tatizo letu watanzania tunanzani watoto wa kitanzania ni washamba sana kila kitu hawawezi. Hivi kutumia OMR ni kitu ambacho wanafunzi wanaweza kushindwa? Ninavyoelewa, karatasi za majibu hupelekwa kwa Maafisa Elimu wa Mikoa, kama wana mashaka na teknolojia si wachukue sampuli wasahihishe kwa mkono? Watanzania ni kulalama na kutafuta visingizio, mwaka jana hawakutumia hizo fomu lakini tulishuhudia wimbi la wasiojua kusoma na kuandika wanaenda sekondari.
Tuangalie kwa kina shule zetu, je walimu wanafundisha au kazi kuwatumia wanafunzi kuwafanyia kazi zap hasa huko vijijini?
Wakaguzi mpoooo mnaona watoto wanavyolkmishwa mashamba??????????

Ni kweli performance ya vijijini ni poor kwa sababu karibu muda wote wanafunzi wanatumikishwa na walimu. Ajira ya watoto bila malipo.
 
.....mchepuo upi anasoma?????

Mwanasha alionekana British Counsel akifanya paper za TOEFL ajili ya college (foundation stage) kama sio USA basi UK ataenda atasoma 2yrs apate credit kuingia College!ukimtafuta baada 5yrs atakuwa ana graduate University na kuja kupata kazi wizara nje au fedha au mashirika UN!
 
Baada ya kuona matokeo ya darasa la saba ufaulu ni chini ya 30% kuna tetesi kuwa wameamua kutumia ya mock kimikoa ili kuficha aibu hii. Walimu walipodai nyongeza walibezwa sana wakiwemo hata baadhi ya wazazi sasa twaona kumbe walimu wameamua kweli na huu ni mwanzo.

Kikwete acha kujifanya huoni okoa jahazi hili,waongeze mshahara walimu inakuwaje wabunge mnawaongeza kwani wanawazidi nini walimu kwa umuhimu? Halafu huyo waziri wa elimu na naibu wake mbona hawatetei walimu ila kuwakandamiza. Kibaya zaidi Waziri wa elimu alishindwa kusimamia wizara ya uchukuzi itakuwa elimu hiv hata kufikiri kidogo rais huwezi?

Sasa mtavuna mlichokipanda endeleeni kueleza mafanikio ya ccm kwa pesa nyingi huku huduma za jamii zikiachwa solemba, rais hauna uchungu hata kidogo na hatima ya Taifa hili kwa vile watoto wako wanasoma shule nzuri. Ogopa kuhukumiwa na historia. kukubali makosa si ujinga. Walimu wamegoma na kama huamini endelea kujidanganya ccm itaondoka kama KANU ya Kenya ilivyoondoka kwa kudharau walimu. Mwalimu hawezi kufundisha akiamua hata kwa vitisho hiv unaweza kumtisha wakati wewe haupo darasani.

Mlienda mahakamani haya sawa mahakama iende kufundisha, bora mgomo wazi kuliko huu baridi
 
JF ya siku inanishangaza sana , kila kitu ni TETESI na unaleta thread kutuaminisha tetesi yako iwe ukweli, JF members tumekosa mwelekeo na tunadharauliwa kila siku. Thread km hizi zamani zimefutwa, kwani hazina hata chembe ya ukweli.
 
Lakini unaelewa maana ya tetesi au ndo wale mnaotaka kubisha tu ili mradi uonekane. Kitu chochote ambacho ni tetesi kinawezakuwa na ukweli ila mstaarabu yeyote huweka kwa tahadhari wakati akiendelea kufanya uchunguzi wewe wa wap? Halafu ikitokea hivyo utajisikiaje?
 
Ama kweli Ukistaajabu ya MUSA Utayaona ya FIRAUNI: "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" Msemo huu ulitikisa sana 2000 hadi 2010 kwa kibwagizo cha "Ari Mpya, Kasi Mpya, Nguvu Mpya" Leo hii imekuwa ni aibu kuutumia ingawa katika kampeni za Mwka jana kuliboreshwa ikawa "Ari Zaidi, Kasi Zaidi, Nguvu Zaidi"

Nikitafakari najiona MJINGA NA MPUMBAVU Mbele ya Jamii ambayo pia inadanganyika kama mimi. Maisha yaliyotabiriwa kwa GHARAMA KUBWA ya mabilioni yamekuwa ni maisha ya kimasikini na taabu nyingi. Sijui tulikosea wapi? Yes nimegundua tulipokosea ni katika kile kisanduku cha kupigia kura. Kwanza tulipewa karatasi za kupigia kura tukaelekezwa kwenda kwenye kisanduku cha kupigia kura huku tukiwa hatuna matumaini ya kesho itakuwaje. Mara maneno ya ahadi tamu yakawa yanajirudia na kutushawishi kwenda na RANGI YA KIJANI KWA AJILI YA MAISHA BORA HAPO BAADAYE. Hakika kwa kuwa sijapata maisha bora nahisi nilitapeliwa na Jakaya Mrisho Kikwete aliyeniahidi kitu ambacho hakunitimizia na hawezi kutimiza hata kabla hajamaliza muda wake.

Matokeo ya darasa la saba ni matokeo ya propaganda za CCM dhidi ya walimu wetu. Katika CV ya Kikwete anaonyesha alisoma Msoga, swali je kama walimu wa wakati ule wangekuwa ndiyo hawa wa sasa ungesoma wewe, je ungekuwa Rais leo wewe. Mama Kikwete ungemuoa akiwa Mwl wewe?

Ushauri kwako, kabla hujamaliza muda wako hakika iboreshe taaluma hii ya UALIMU vinginevyo wewe ndiye Rais na ndiye muangamizaji wa ELIMU NCHINI kama hutaboresha sekta hii kabla ya 2015.
Kama unayonia ya kukiendeleza chama chako cha CCM basi fanya hivyo lakini kama unaagenda za kukiua chama chako cha CCM tulia kama maji mtungini.
 
serikali ya jakaya na ccm wameona elimu ni ghali hivyo wamejaribu ujinga na tunasubiri wazir atangaze matokeo halafu kwa ujinga wa walio wengi wataunga kauli ya waziri mkono. The nation is dying silently.
 
Wanaweza kila kitu hata kulima na kutumikishwa kwingine wanaweza sasa mbona nawe unalalamika? Kwani kutumikishwa, kulimishwa hasa huko vijijini nayo si sehemu ya elimu, hasa elimu ya kujitegemea.....

Naamini binadamu yeyote mwenye akili timamu ana uwezo wa kufanya chochote hata kile ambacho hajawahi kufikiria kama anaweza kukifanya ilimradi amepatiwa mafunzo sahihi! Nilichosema si kulalamika bali ni kuelezea ukweli halisi na ninaendelea kuamini kwamba kwa aina ya vivuli (photocopy) vya fomu nilivyoviona wanagu mwenyewe wakitumia kama sehemu ya mazoezi, ni wazi kwamba hata baadhi ya walimu wao ambao hawakupata fursa ya kushiriki katika sensa hii na iliyotangulia, watakuwa walizishangaa fomu halisi za OMR zilizotumika katika mitihani ya wanafunzi wao mwaka huu!! Naomba isieleweke vibaya kwamba kushangaa ni sawa na ushamba, lahasha, ni ukweli usiopingika kwamba teknolojia hii hapa kwetu haijazoeleka kiasi cha kuzikuta karatasi za namna hii pahali pengi. Hivyo naendelea kuamini ikiwa baadhi ya watoto wetu waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu hawakupata fursa mapema ya kuziona na pengine kuzifanyia majaribio karatasi halisi za OMR tutarajie kiwango cha kufeli kuongezeka na mojawapo ya sababu ni teknolojia.

Ili kuepusha hili karatasi za rough walizofanyia kazi hasa kwa mitihani kama ya hisabati na mingine yenye asili hiyo, ni lazima zikasahihishwe na hili linaweza kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa katika kutoa matokeo. Watoto wetu wa siku hizi wa darasa la saba wengi ni wadogo kuweza kumudu umakini wa hali ya juu unaotakiwa katika kujaza fomu za kusomwa na mashine sensitive kama za OMR....

kaka nimekusoma. Hata hivyo, yaelekea wewe ndio una mashaka wala si watoto au walimu wao kuhusu uwezo wa kutumia fomu za OMR. Wanafunzi wetu waliweza kutumia fomu hizo na wala tatizo la kushuka kwa matokeo sidhani kuwa linatokana na watoto kutotumia vema fomu husika. naona ukweli tusiukwepe ni uwezo duni kitaaluma walionao watoto wetu sasa unaotokana na kutofundishwa ipasavyo madarasani na walimu waliovunjika moyo wa kazi baada ya kutelekezwa na serikali yao muda mrefu. period.
 
Back
Top Bottom