Ndio maana kuna swali nilijiuliza, hivi hii siku yetu ya uhuru na Zanzibar inasherehekewa? na kule kwao ni mapumziko kama huku bara? kama na Zanzibar wanasherehekea, vipi yale mapinduzi yao "matukufu" wanayaweka kwenye nafasi ipi?
Au ndio maana nasi huwa tunasherekea siku ya mapinduzi ya Zanzibar? kwamba tuko ndugu moja, lako langu... langu lako? anyway, hata kama ndio hivyo, sioni kosa kwanini hii siku ya uhuru isiitwe siku ya uhuru wa Tanganyika, sio Tanzania, naona iitwe hivyo hata kama itasherehekewa pande zote mbili.
Kumbe huwa kuna kosa la kiufundi linarudiwa kila mwaka kwenye maadhimisho ya hii siku, ni vyema sasa wahusika waamke.