Darasa: Maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika!

Utopolo tupu
 
ushahindi wa kisheria au kikatiba au mikataba wa kuifuta Tanganyika.
Kwa taarifa waziri wa TAMISEMI wa tanganyika mwisho Chumbe.
 
Tnapendaga sana kulazimisha UJINGA kwa vitu very simple yani

Hivi leo tukisimama kwenye FACT na kutambua leo ni siku ya uhuru wa TANGANYIKA tutaharibu au kupungukiwa na nini?

Iwe kama ilivyo sahihi kwa Zanzibar kutambua siku ya MAPINDUZI

Sherehe yetu ya Muungano ndio ibaki kama sherehe ya kutambua kuzaliwa kwa TANZANIA

Kwa kumbu kumbu nzuri zaidi ya viza vijavyo ni vyema zaidi tuka ainisha haya mambo vizuri na kwa ufasaha wake kuliko kulazimisha KUUA kabisa utambulisho wa TANGANYIKA kwenye historia ya kusherehekea uhuru

Mifano ya Pasco ni ya kitoto sana na haiwezi kurandana na swala hili abadani

Hakuna nchi inayoitwa Tanzania iliopata uhuru that day
Leo ni siku ya UHURU WA TANGANYIKA........ Periode
 
Zanzibar ilipata uhuru wake December 1963 kutoka kwa mwingereza. Uhuru ulikabidhiwa kwa Sultan wa Zanzibar aliyewakilisha Monarch ya Oman Sultanate.
Mapinduzi ya Zanzibar ya April 1964 ni Matokeo tu ya janja janja iliyofanyika kati ya viongozi wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Zanzibar ni kwa heri ukoloni ,kwa heri uhuru.Uhuru wa Zanzibar ungeadhimishwa kesho yaan 10/12/2021,Ila kwakuwa uhuru huo ulipinduliwa ndo maana hata hiyo tarehe tu haitajwi.Waliopindua wanalinda uhalali wa udhalimu walioufanya kwa sababu wazijuao wao.
 
Tanzania ilipata uhuru lini
 
Katiba iliyoipa Zanzibar uhuru 10/12/1963 ilijadiliwa na serikali ya mseto wa ZNP na ZPPP kwa upande mmoja na serikali ya Uingereza kwa upande mwingine.Vyama vyote pamoja na ASP vikimtambua sultan kama mkuu wa nchi na ndo maana vilisajiriwa na kufanya siasa.ASP walipopata support ya jamaa fulani wa kashirikiana na wahuni wakaipindua serikali halali.Katiba ikafutwa na Karume akatoa amri hakuna Uchaguzi Zanzibar hadi 2030.
 
Ni Uhuru wa Tanganyika.

Tanzania ni pamoja na Zanzibar ambao wao wanasherehekea 12 January.

Tanzania haijawahi kupata Uhuru bali ilipata katiba yake mwaka 1977
Hizo sherehe zote ni Feki,hata hiyo ya Zanzibar siyo ya kusherehekea uhuru wa Zanzibar,tarehe 12/1/1964,ni siku mbaya kabisa kwa taifa la Zanzibar,ni siku ya uvamizi na iliyochafua kabisa taifa huru la Zanzibar.
 
RUMENYA ni hali ya mtoto wa kiume kuhamia kwa mwanamke.Hali ya Tanganyika kujiimilikisha mazima kwa Zanzibar inaitwaje?
 
Watu ukweli wanaujua, Ila kwa vile hatuko HURU ndiyo maana tunaogopa kusema ukweli. Leo Ni Uhuru wa Tanganyika. Kuna siku tutasherehekea UHURU wa Tanganyika. Huu ipuuzi wa leo ni mauzauza ya wanasiasa. KUNA SIKU UKWELI UTASIMAMA NA TANGANYIKA ITASHEREHEKEA UHURU WAKE
 
Hujui kitu chochote ina wezekana wew ni kima
 
Beatrice umeeleweka, sijui ni kwa nini watu tena wasomi wabobezi wanatumia nguvu nyingi, ulaghai na hila lukuki kutaka kuipoteza Tanganyika kwenye uso wa dunia wakati ilijipata uhuru wake tar 09 Disemba 1961. Kwani iliwakosea nini Tanganyika yetu!
 
Kitu najifunza hadi sasa ni kuwa tumepoteza historia yetu kwa ujinga wetu wenyewe, leo mzee wangu Mayalla anasema ni uhuru wa Tanzania taifa ambalo halijawahi kuwa koloni la mtu.

Ni kama tulivyosoma na wanavyosoma vizazi kuwa Tanganyika ilikuwa koloni la muingereza, kitu ambacho sio kweli, ni makusudi tu zimetumika.

Wapo waliokuja na wakasema bendera ya Tanzania ina rangi nyeudi, kijani, bluu na njano, wakati hakuna rangi ya njano kwenye bendera ya Tanzania, na hawa wameaminika hadi na watawala, inashangaza sana. Ukiwaambia bendera ina rangi ya dhahabu/gold na sio njano watakukatalia, ila uzuri sheria ya Bendera inaeleza wazi wazi.

Kuna kila sababu yakurudi nyuma kuangalia mitahala yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…