Dark days 17/03/20...

Late CEO alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa CEO bora kuliko wote. Sijui nini kilimchanganya. Mwisho wa siku amekuja kuonekana wa kiwango cha chini sana hadi Born Town anaonekana wa maana.
 
Acha kutupiga fix, wa mabilioni biashara hawalipi kodi wengi. Ujanja ujanja tu kama ilivyo sasa hivi
 
Najiuliza tu kwa sauti....hadi lini mtaendelea kuwaondoa manabii wenu wenyewe?

Kama hawa wenye kampuni wananisikia, uzalendo wao ungekuwepo wangeuonyesha kwenye kuwaondoa wanaohujumu uchumi wakishirikiana na mabeberu mchana kweupe; lakini kwa kumwondoa yule ambaye mnampakazia sasa ili kuji justify kwa uovu wenu mlioutenda, damu yake itawalilia mpaka vizazi vya 10 vya viuno vyenu.

However all things work together for good...It is well with My country!
 
Late CEO alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa CEO bora kuliko wote. Sijui nini kilimchanganya. Mwisho wa siku amekuja kuonekana wa kiwango cha chini sana hadi Born Town anaonekana wa maana.
Bado atakuwa ndiye....Tatizo matarishi ambao bado wanaendeleza ukoloni mambo leo wanataka kutuaminisha wanachopenda tuamini...Mie kwa hili nafsi yangu haitakaa iwaelewe hata nikilazimisha ielewe...Ipo siku mtajua hamjui!
 
Acha kutupiga fix, wa mabilioni biashara hawalipi kodi wengi. Ujanja ujanja tu kama ilivyo sasa hivi
Ndio maana mliunda kikosi kazi ili muuwe biashara za watu eeeeh?

Pale TRA wapo wengi walichukia kikosi kazi kukaa pembeni... Kamuulizie H. Sali.. Yupo analia na mshahara tuu baada ya kikosi kazi kuvunjwa... Watu walikuwa na uhakika wa mpaka million mbili kwa siku... Za Rushwa.... Mnavamia wafanyabiashara wakubwa kwakuwa mna go ahead (ruhusa ya Jiwe) mnawaambia toa kiasi hiki TRA.. Na mimi nipe kiasi hiki... Bila hivyo jiandae kwenda Kisutu na nitahakikisha hakuna dhamana.....

Ilikuwa wakati wenu kutesa... Sasa yalishapita hayo...
 
Ila Jiwe pamoja na mazuri yake baadhi hasa kuboresha Miundombinu nchini ila alikua na ROHO mbaya sana .
Alikua na ile nile mimi tu na wanaonisifia ,wengi walimuweza kwa kumsifia kinafiki walinde ugali.
Yule bwana tungekua na Tanzania huru yenye mikakati ilifaa awe Waziri wa Ujenzi kama alivyokua ila sio mbeba maono .
 
Late CEO alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa CEO bora kuliko wote. Sijui nini kilimchanganya. Mwisho wa siku amekuja kuonekana wa kiwango cha chini sana hadi Born Town anaonekana wa maana.
Mtu mshauri wake Mkuu Paulo na Slowslow lazima kuna mahala utakosea ….Born Town ni zao la System hata washauri wake na watu wanaomzunguka ni haohao hapo ndo difference ilipo
 
Nani kakuambia nipo serikalini!!!! Au kwa hata kufanya kazi na lolote la umma!!! Karibu kijijini tulime.. hao wasema nikawaulize mimi haya yote yananihusu nini? Duh!!!
 
Hehehe
 
Mimi unafikir nakubaliana na ccm hata kwa bahati mbaya jinsi wanavyoendesha hii nchi? Hapana. Natamani reformation kubwa sana lkn siyo kwa kuuana. Hicho kisasi chake achaaa. Nakuambia hicho kisasi ysikitamani. I know there are smart ways to deal with this. Ila siyo kwa kuua. Its never the best option.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Late CEO alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa CEO bora kuliko wote. Sijui nini kilimchanganya. Mwisho wa siku amekuja kuonekana wa kiwango cha chini sana hadi Born Town anaonekana wa maana.
Tatizo lake alikuwa materialist ndio hapa alianza kujichanganya, yeye alipenda vitu bila kuviwekea misingi ya utu na uwazi. Kwa mfano issue ya elimu bure alikurupuka maana nchi yetu bado ni changa haina financial supremacy kutoa free service. Leo ukienda kwenye shule zetu unalia, hali mbaya sana. Badala ya kuboresha elimu yeye alipenda sifa zaidi.

Kiongozi sio kujenga madaraja na kutunisha misuli. Kwenye dunia ya leo unadanganya watu kwa unaweletea maendeleo badala ya kuwajengea uwezo wajiendeleze wenyewe. Mzee alikuwa mtendaji ila hakuwa kiongozi mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…