Kwangu mimi ukabila alioanzisha JPM umefuta mazuri yote aliyofanya. Ubabe wa kuwafungia wafanyabiashara akaunti za benki. Mtu anaacha kuwafungia akaunti wanasiasa waliopita anakazana na wafanyabaishara. Rais wa kwanza kuweka kipaumbele alipozaliwa mpaka kujenga Uwanja wa ndege wa kimataifa. Hela zote zilizotumika haziwezi kurudi. Kila miradi aliijenga haukuwa na mipango thabiti. Hakuna ajira zilizozalishwa. Mama huyu anaomba kutoka kwa JPM hakuna mtu anaongea kuhusu Kizimkazi kwa sababu tushazoea alichofanya JPM Chato. Hakuna mtu anaongea kuhusu wazanzibari kwa sababu JPM alishatuzoesha kuhusu wasukuma.Tukitaka tuendelee inabidi mapinduzi makubwa yafanywe ndani ya CCM.JPM ndiye aliyeanzisha teuzi zisizokuwa na sifa. Wakuu wa wilaya na mikoa wasio na vigezo na sifa. Na mama analiendeleza hilo.
Kwa kusoma hii kauli naweza kuhisi unatokea sehemu gani ya Tanzania.
Kusema ukweli mna ubinafsi sana na ndo maana watu wanaogopa sana kuchagua kiongozi kutoka
ukanda wenu. Kwenu hamkuendelea kwa juhudi zenu tuu,ni juhudi za wote watanzania wavuja jasho.
Ila viongozi waliangalia vipaumbele ili kuinua uchumi wa nchi mkadhani ni juhudi zenu binafsi.
Hivi mnaona ni sawa kwenu mnafungulia maji kwenye bomba wengine wanakunywa kwenye kisima cha mifugo?
Ipi bora,mtu aendeleze kwao ambako ni sehemu ya Tanzania iliyosaahulika,au ajenge mahoteli na vitegauchumi
vingine nje ya nchi ambapo havichangii hata kidogo uchumi wa taifa wala kusaidia mwananchi?
Sasa magu hayupo,niambie kipi kimebadirika? Kama ni siasa.aliyewakimbiza wazanzibar wakakimbilia mombasa
alikuwa magu? Aliyesema ndege ya rais itanunuliwa hata kama mnakula pumba alikuwa magu?
Aliyefanya upigaji wa rada si angejenga kwao walau watz waone rami kwao?
Shida yetu hatujui tunachokihitaji badala yake tunakimbizana na tusichokijua
mwisho wa siku tunajikuta tumechoka na mikononi hatuna kitu.
Ubaya wa ni kwamba Magu hakuwa mnafiki alifanya alichokiamini hadharani ,na hapa ndo wengi walimchukia kwani alipokasirika alionyesha
wazi wazi. Lakini waliopoka haki za wastaafu na madaktari na kisha
kumteka na kumtesa dokta ulimboka,kwa kuwa hawakusema lolote ila wakamuumiza
tunawachekea na kuwasifu na hapa ndo kisa cha lindi la umaskini wetu.