Ninaweza kukubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo ambayo majeshi yetu huyafanya pasipo watu wengine kujua. Tanzania imefanya operations nyingi sana na zenye mafanikio makubwa. Hata hili la kumuonyesha bwana Paka ni mjanja wa Intelijiensia lina sababu zake na kwa maksudi maalumu.
Kipindi kile cha 2014 alivyojifanya kwamba anaweza kuipiga kampuni yetu, watu wetu wa kazi waliweka mitambo kwenye kakichuguu na wakawa wanaichungulia kampuni yake.
Wakati anawaza kuipiga kampuni yetu tayari vijana wetu wa kazi walishahamisha baadhi ya watu wetu na kutengeneza shelters ili akirusha tu hakuna raia hata mmoja, sasa ushangae kule kwake hakuwa amejipanga hivyo, so angeleta madhara makubwa kwa wananchi wake na kampuni yake.
But thanks God alipigwa kwa diplomasia tu.Jamani fuatilieni historia ya nchi yetu, ni nzuri sana n ya kusimumua, ukiijua mtu hawezi kukudanganya kwamba tu dhaifu. Tuko imara sana.
Kitu kingine ambacho hakujua alidhani infos alizonazo zimemtosha kuijua kampuni yetu, kumbe hakuwa anajua kama alivyojiaminisha, alijua vichache huku vijana wa kampuni yetu wakijua mengi ya kwake.
Kampuni yetu siyo hivyo jinsi ilivyo madhaifu yetu ya ndani haina maana kwamba hata huko nje ndivyo tulivyo. Siyo kila mlevi amelewa. Mambo mengi huachwa hivyo hivyo kwa maksudi.
Kule porini kuna mambo nyinyi acheni kabisa, mmewahi kusikia pango la wanyang'anyi ambalo lilikuwa likifanya uharamia? Linavamia watu linaiba mbuzi,ng'ombe, kuku, bata mpaka nafaka kisha wanatumwa wazawa kwenda kusaga halafu wanawapelekea kwa kuogopa kuuawa?
Hili genge lilijiona untouchable wakati huo, walikuwa ni wengi kama kijiji, kuna wake, watoto na watu wengine kibao wanaoshirikiana nao, mnajua walifanywa nini?
Saa 2 za usiku ,walijikuta wamefukiwa pasipo kusema hata kwaheri, na mnajua kwanini ilikuwa ni saa 2 za usiku? Kwasababu ulikuwa muda wa msosi wa usiku wamekusanyika pamoja.
Kisa kingine huko huko,majambazi yalikuwa yamejificha porini na yameleta usumbufu mkubwa sana, kila yakitafutwa hayaonekani lakini utekaji unaendelea.
Akatumwa Komandoo mmoja kutoka JWTZ wakamdrop porini akaanza kuwatafuta, ghafla hawa hapa, akawasoma na kujua idadi yao, nao bwana vile vile wanaota moto wamejikusanya. Alipiga risasi moja kwenye ule moto si mnajua baruti na moto. It was the end.
Watanzania wenzangu JWTZ, TISS na POLISI ni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo viko imara sana hizi changamoto za ndani zisitufanye tukose navyo amani, vinafanya kazi nzuri sana ila kwa kuwa hazitangazwi si rahisi kujulikana. (Hawa wachache wanaoharibu ndio waondolewe)
Mambo yao ni mengi hapa nimeandika kwa ufupi tu. Kama nilivyosema huyu mtu huenda anapaishwa tu lakini kwamba ana nguvu kiasi cha kutupangia cha kufanya sidhani kwa jinsi ninavyoijua na ninavyoielewa nchi yetu kwa historia yake.