Madwari Madwari
JF-Expert Member
- Sep 16, 2014
- 1,825
- 3,085
Nimekaa nimeusoma huu uzi baada kusikiliza interview ya Mo Dewji nimekuja kugundua kuna umuhimu wa kuwa na team imara katika kuiongoza nchi. Uongozi wa Borntown ukikuwa na kasoro zake lakini ulikuwa na team imara. Ukiangalia Late CEO na New CEO hawana team. Unaona kabisa maafisa wa serikali wanakinzana na kila mtu anatoa maagizo. Hichi kitu kinaharibu nchi na kinatengeneza mapengo makubwa sana ya kuruhusu mambo kufanyika bila uongozi kujua. Mara mia Borntown na Mamvi wangemaliza tofauti zao na kumruhusu Mamvi agombee 2015. Ukisoma magazeti na ukiangalia taarifa ya habari unaona kabisa viongozi hawafanyi kazi pamoja. Inabidi CCM ikae chini na iunde team ya watu makini bila kuangalia ushabiki. Iundwe team ya watu wenye uwezo, inashangaza sana kuona viongozi wanateuliwa kichawa. Ukiangalia CV za wateule wetu unaweza ukashindwa kumshauri mwanao asome au akazane na mbio za mwenge. Pengine akikomaa na mbio za mwenge anaweza akapata hata ukuu wa wilaya.