Nchi hii kuna matatizo makubwa sana ya kuondoa umasikini, maradhi na ujinga; sasa kuna panya road wameibuka kama zao la ukosefu wa ajira (shughuli za vijana kufanya wapate mkate wa kila siku);
haya yote hayajapata ufumbuzi, watu wako busy na nani apite kwenye barabara ya mwendo kasi.
Surprisingly, ukitoa magari ya mwendokas yanayopita ambayo yamebeba walalahoi, wanaogombania kupita kwenye barabara na magari yao wengi na wenye mamlaka. Picha zinazosambaa au walio barabarani wanaona nani anaekatiza kinyume cha sheria.
Kuna shida sana nchi, mambo major kama kuhakikisha Dar na Tanzania inakuwa sehemu salama ya kuishi, taasisi za umma zinatunishiana misuli barabarani.
Mawaziri wa kisekta wako wapi kutoa mwelekeo kwa manufaa ya umma wa Watanzania?
Badala ya kuwa na mjadala mkali na huru wa hatua za msingi zifanyike kuongeza magari barabarani kwa lengo la kuboresha usafiri, abiria wake na magari yawe yanaondoka vituoni kwa muda na abiria wote wawe wameketi kwenye viti, story iliyopo ni kama funika kombe mjadala wa kufuta tozo uishe.
Nchi hii, tuna safari ndefu kweli